Katika ile hali ya kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2017, Timu ya Boko Beach Veterans (BBV) iliandaa mechi ya kirafiki baina ya BBV Basheka na BBV Kilimba mchezo uliopigwa katika uwanja wa BBV, Boko Jijini Dar es salaam. Mchezo huo ambao ulikuwa ni wa kuvutia sana kwa timu zote kucheza kwa kushambuliana kwa zamu, ulimalizika kwa timu ya BBV Basheka kuibuka na ushindi mnono wa bao 3-0 dhidi ya wapinzani wao, BBV Kilimba.
 Kikosi cha BBV Basheka.
 Kikosi cha BBV Kilimba.
Mshambuliaji wa pembeni wa BBV Basheka, Juma Ndambile akijiandaa kuachia shuti kali kuelekea lango la wapinzani wao, BBV Kilimba, katika mchezo wa kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2017 uliopigwa katika uwanja wa BBV, Boko Jijini Dar es salaam jana.
Kiungo mchezeshaji wa  BBV Kilimba, Tippo Athuman a.k.a Zizzou akiichambua vilivyo ngome ya BBV Basheka, katika mchezo wa kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2017 uliopigwa katika uwanja wa BBV, Boko Jijini Dar es salaam jana.

Mshambuliji tegemeo wa BBV Kilimba, Messi akiondoka na mpira kuelekeza shambulizi langoni mwa wapinzani wao, katika mchezo wa kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2017 uliopigwa katika uwanja wa BBV, Boko Jijini Dar es salaam jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...