Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge akiwa katika boti ya kisasa inayotumiwa na idara ya maliasili na uvuvi wilaya ya Nyasa kabla ya kuzunguka ziwa Nyasa kuangalia vivutio mbalimbali vya utalii katika wilaya ya Nyasa mkoani humo,kushoto ni mkuu wa wilaya ya Nyasa Esabila Chilumba.
Naibu waziri wa elimu na mafunzo mhandisi Stella Manyanya kushoto akimsikiliza askofu wa kanisa la Anglikana Doyasisi ya Ruvuma Raphael Reuben Haule ndani ya boti la Mv Matema linalofanya safari zake kati ya kijiji cha Liuli na maeneo mengine ndani ya ziwa Nyasa,katikati mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge katikati akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Tamasha la kuvitangaza vivuutio vya utalii katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma jana,kulia mkuu wa wilaya ya Mbinga Kosmas Nshenye,wa pili kulia mkuu wa wilaya ya Nyasa Esabila Chilumba na kushoto nmbunge wa jimbo la Nyasa Stella Manyanya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...