Baraza maalum la madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, limejadili na kupitisha mapendekezo ya bajeti ya halmshauri hiyo, yenye jumla ya Sh. bilioni 60.7 kwa mwaka wa fedha wa 2017- 2018 huku kiasi kikubwa cha fedha hiyo ikikielekezwa kwenye miradi ya maendeleo.
Taarifa iliyotolewa na kitengo cha habari na mawasilino cha halmshauri ya Wilaya ya Mufindi, imebainisha sehemu kuu mbili za bajeti hiyo, ambapo jumla ya shilingi bilioni 4.9 zimetengwa kwa matumizi ya kawaida, wakati bilioni 14.5 zikielekezwa kwenye miradi ya maendeleo.
Taarifa hiyo imevitaja vyanzo vya mapato hayo, kuwa ni makusanyo ya halmashauri, fedha kutoka serikali kuu, wafadhili, taasisi za kijamii sanjari na nguvu za wananchi.
Akizungumza wakati wa kuhailisha kikao hicho, mwenyekiti wa halmshauri ya wilaya ya Mufindi Mh. Festo Mgina amemtaka Mkurugenzi mtendaji pamoja na wataalamu wake kuhakikisha wanaisimamia na kuitetea bajeti kwa hoja zenye mashiko katika ngazi ya Mkoa na Taifa ili malengo ya kuharakisha maendeleo ya halmashauri yafikiwe kwa wakati na akawahimiza watumishi na madiwani kushirikiana katika ukusanyaji wa mapato.
Kupitishwa kwa bajeti ya na baraza la madiwani, ni kwa mujibu wa sheria ya fedha yaserikali za mitaa namba 9 ya mwaka 2013. Aidha bajeti hiyo imezingatia mwangozo wa kitaifa wa bajeti wa 2017/ 2018, ilani ya uchaguzi ya chama tawala CCM ya 2015/2020, mpango wa maendeleo wa Taifa wa mwaka 2017/2018 huku mambo mengine yakiwa ni malengo ya maendeleo endelevu, dira ya Taifa ya maendeleo 2025 pamaja na maelekezo ya kisekta na mpango wa maendeleo ya miaka mitano.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...