Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ally Hapi leo ametembelea kituo cha
Polisi cha Msimbazi jijini Dar es salaam ambacho kilipatwa na ajali ya
moto siku za hivi karibuni na kutoa msaada wa mifuko 100 ya saruji sawa
na tani 5.
Katika ziara yake kwenye kituo hicho, Hapi ametembelea kambi ya makazi ya askari na familia zao iliyoko nyuma ya kituo hicho ambapo amekabidhi mifuko hiyo ya Saruji kwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala Ernest Matiku na kuagiza kuwa saruji hiyo itumike kwa ukarabati wa jengo zima la kambi hiyo ambayo inakaliwa na familia 72 za askari.

Kaimu Mkuu wa Mkoa ameeleza kuwa Polisi wanafanya kazi kubwa ya kulinda amani na usalama na hivyo jamii haina budi kuwaunga mkono.
Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Ilala Ernest Matiku ameeleza kuwa wanamshukuru Kaimu Mkuu wa Mkoa kwa msaada huo kwani jengo lao limechakaa sana hali inayohatarisha usalama wa askari na familia zao.Hivyo wataanza ukarabati mara moja vifaa vitakapo kamilika na kila kitu kitafanyika kama ilivyo kusudiwa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...