Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MWANAMUZIKI wa muziki wa kizazi kipya Benard Paul 'Ben Pol, ameachia wimbo mpya unaoitwa 'Phone' akimshirikisha mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Mr. Eazi.
Akizungumza kuhusiana na kuachiia wimbo huo mwanzoni mwa mwaka Ben Pol amesema kuwa wimbo huo ameutengeneza katika studio ya One love records, iliyopo jijini Dar es Salaam chini ya mtayarishaji Tiddy Hotter.
Ben Pol alisema ujio wa wimbo huo ni moja ya mipango yake ya mwaka 2017 na ameanza kwa kutoa wimbo huo wa 'Phone'. na tayari wimbo huo umeanza kusikika kupitia vituo mbalimbali vya radio, huku ujio wa video yake ukiwa njiani.
"Wimbo wa Phone ni moja ya malengo yangu ya mwaka huu na ndiyo ujio wangu wa 2017, naomba wapenzi waupokee na kuusikiliza kila mtu ataelewa nini nimejipanga kupitia mwaka huu"alisema Pol.
Mwanamuziki huyo anayetamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo pamoja na, Moyo Mashine, Maneno, Sofia, Pete, Maumivu, Samboira na ameshirikishwa kwenye wimbo wa Darasa unaotamba kwa sasa nchini unaitwa muziki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...