Afisa Biashara wa jiji la Arusha, Steven Sultan(wa pili kulia) na Meneja wa
Huawei jijini Arusha,Qin Yilin(wapili kushoto) wakikata utepe kuashilia uzinduzi
wa duka la Huawei Skytel uliofanyika jana jijini Arusha.Kuhoto ni Meneja Huawei
Kanda Kanda ya Kaskazini, Betrice Vitalis.
Afisa Biashara wa jiji la Arusha, Steven Sultan(wa pili kulia) na Meneja wa
Huawei jijini Arusha,Qin Yilin(wapili kushoto) wakipongezana kwa kushikana
mikono mara baada ya kukata utepe kuashilia uzinduzi wa duka la Huawei Skytel
uliofanyika jana jijini Arusha.Kuhoto ni Meneja Huawei Kanda Kanda ya
Kaskazini, Betrice Vitalis.
Meneja Huawei Kanda Kanda ya Kaskazini, Betrice Vitalis(kushoto) akitoa
maelekezo ya bidhaa za Huawei kwa fisa Biashara wa jiji la Arusha, Steven
Sultan mara baada ya uzinduzi wa Duka ka Huawei Skytel kuzinduliwa rasmi
jijini Arusha.Kulia ni Meneja wa Huawei jijini Arusha,Qin Yilin na
Mkurugenzi wa Duka hilo, Bobkevin Shoo.
Kampuni ya Teknolojia ya Mawasiliano ya Huawei Tanzania
kwa kushirikiana na Mfanyabiashara maarufu wa simu jijini Arusha, Skytel
wamefungua duka kubwa liitwalo “ Huawei Skytel Brand Shop” katika Jiji la
Arusha. Hatua hiyo ni mwendelezo wa Huawei katika kutekeleza moja ya mikakati
yake ya kujitanua kibiashara nchini.
Huawei imeona kuwepo wa Duka hili kubwa la Skytel, katika Jiji la Arusha
kunatokana na kukua mahitaji ya bidhaa za Huawei nchini na hivyo kutoa fursa ya
watumiaji kupata huduma kwa karibu zaidi.
“Tunafahamu watanzania walio wengi wanachohitaji, ndiyo maana leo hii tuko
Jijini Arusha. Tunaamini kuwa hii ni fursa pekee kwa wakazi wa Arusha na miji ya
jirani kupata bidhaa zetu zenye ubora na viwango vya hali ya juu. Tunaamini kuwa
Skytel wana jina kubwa katika Jiji la Arusha na hivyo itatusaidia sisi kutimiza
lengo letu, alisema Meneja wa Huawei jijini Arusha,Qin Yilin.
Mwaka huu kampuni hii ya simu ilijipanga kusambaza huduma yao nchi nzima,
sambamba na kufungua maduka kwaajili ya kusogeza huduma zetu kwa wateja.
Hali hii imetuongezea wepesi wa utoaji wa huduma zao kwa kufanikiwa kwa kiasi
kikubwa kutambua mahitaji muhimu kwa wateja wetu,
Tanzania imefaidika na uhusiano mzuri uliopo kati yake na Huawei kwa kuwa na
miradi mbalimbali yenye lengo la kuboresha teknolojia ya mawasiliano. Huawei
inampango wa kukuza teknolojia ya mawasiliano nchini Tanzania na sasa imeanza
kushirikiaba kwa karibu na wazawa kama Skytel. Milango iko wazi kwa yeyote
anayetaka kutuunga mkono kiabiashara.
Wakati Huawei inazindua duka hilo katika Ukanda wa Kanda Kaskazini, Meneja
wa Huawei Arusha alitangaza uwepo wa simu mpya ya kisasa, Huawei Y3II na
nyinginezo, katika soko la simu nchini.
Alisema kuwa simu hiyo ina ubora na kuwataka watanzania kutumia, akifafanua
zaidi kuwa ni simu yenye ubora, lakini gharama yake sio kubwa, ikilinganishwa na
simu za makampuni mengine.Pia bidhaa nyingine zitaambatana na simu hiyo kama
matoleo mangine tofauti Huawei P9, Y3c, Y5II ,Y6II, Y3lite na nyingine nyingi.
Hizi ndizo faida za kuwa na duka kubwa katika Jiji la Arusha. Kuanzia sasa
wanunuzi wa bidhaa zetu wana fursa ya kupata bidhaa zetu zote kwa wakati.
Tunaanza na simu hii ya Huawei Y3II ambayo kwa hakika kila atakayeamua
kuitumia ataipenda kwa ubora wake.
Kwa mujibu wa Meneja huyo, Kampuni ya Huawei inaendelea na mchakato wake
wa kusogeza huduma zake kwa wateja wake, kwa lengo la kutimiza malengo yake
ili kupambana na soko la mawasiliano.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...