Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii Malinyi.
Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ni moja ya Wilaya mpya hapa nchini zilizoundwa kutokana na ukubwa wa mkoa wa Morogoro kwa lengo la kuzidi kuongeza huduma za kiserikali kwa wananchi walio pembezoni hili kupunguza gharama za wananchi kutembea umbali mrefu.
Malinyi ambayo imezaliwa kutoka katika Wilaya Mama ya Halamashauri ya Wilaya ya Ulanga ambayo ilionekana kubwa kuliko kawaida na kushindwa kukidhi kuwahudumia wakazi wa malinyi kutokana na umbali wa kijiografia.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ,Marcelin Ndimbwa, akikagua ujenzi wa madarasa ambayo yamejengwa kwa ajli ya watoto wa wafugaji Rumbanga.
Marceline Ndimbwa ni Mkurugenzi wa kwanza katika halmashauri hiyo mpya kuteuliwa na Rais wa awamu ya tano Daktari John Pombe Magufuli ili kuhakikisha maendeleo ya wilaya hiyo yanafanana na sehemu nyingine.
Ndimbwa amekuwa ni mkurugenzi wa halamashauri hiyo huku akikabiliana na changamoto kubwa ya mgogoro wa ardhi baina ya wakulima na wafugaji na changamoto ya miundombinu ya elimu katika jamii kubwa ya wafugaji.
Ndimbwa anasema kuwa Rumbanga ni moja ya maeneo ambayo hayapo mbali na mji wa Malinyi lakini yamekuwa na jamii kubwa ya wafugaji wa kabila la kisukuma huku wakiwa na changamoto ya kutokuwa na shule ya msingi, Sekondari na huduma za afya.
Ndimbwa anasema kuwa mbali na changamoto zote hizo lakini ameamua kuanza na changamoto kubwa ya kutokuwepo na shule ya msingi katika eneo hilo la Rumbanga.
“kiukweli hali sio nzuri katika eneo la Rumbanga kwani shule iliyopo ni ya nyasi ambayo imejengwa na wanakijiji wenyewe na haina walimu wa kufundisha zaidi ya vijana wawili ambao wamemaliza kidato cha nne na kuamua kujitolea katika kuwafundisha wadogo zao ambao wapo kuanzia darasa la kwanza mpaka la nne”amesema Ndimbwa.
Ndimbwa anasema kuwa mara baada ya kuona mazingira hayo wakaona ni lazima wa kuamua kujenga shule hiyo kuwa ya kisasa kutokana changamoto ya umbali kufata shule ambayo ipo kilometa 34 kutoka hapo Rumbanga na wanafunzi hao kutakiwa kutembea kwenda na kurudi katika shule ya msingi Mwembeni hali iliyochangia watoto wengi kuacha masomo na watoto wa kike kupata ujauzito katikati ya masomo na kulazimika kuacha shule.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...