GWIJI wa muziki dansi nchini 'Kamarade' Ally Choki yuko mbioni kuitosa bendi yake ya The African Stars 'Twanga Pepeta' baada kutengewa 'mkwanja' mnene na bendi ya Extra Peramiho ya Mjini Songea Mkoani Ruvuma. 

Habari za uhakika kutoka mjini Songea zinaeleza, Choki akiwa mjini humo wiki iliyopita alikokwenda kutumbuiza na Twanga Pepeta wakati wa sikukuu ya Krisimasi aliitwa mezani na tajiri wa Extra Peramiho mfanyabiashara John Floyd Ngonyani ili kuweka mambo sawa. 

Taarifa zinaeleza,katika kikao hicho cha siri kilichofanyika katika moja ya hoteli za Kitalii mjini humo Choki, alimueleza Ngonyani kuwa bado ana mkataba na Twanga Pepeta unaofikia ukomo mwakani hivyo itakuwa ngumu kwake kuitosa bendi hiyo kutokana na kubanwa kisheria. 

Inaelezwa mfanyabiashara huyo alimueleza Choki yuko tayari kuvunja mkataba huo kwa gharama yoyote kwani amepanga kuiimarisha Extra Peramiho kuwa moja ya bendi kubwa za muziki wa dansi nchini. Tayari bendi hiyo imeshawanyakuwa baadhi ya wanamuziki waliowahi kufanya kazi na Choki enzi ya Extra Bongo wakiongozwa na kiongozi Greyson Semsekwa na Bob Kisa ambapo wako mbioni kuwanasa mpiga dramu Sunday Mashine na mpiga solo mahiri Ephraim Joshua,Mfaume Solo na mpiga Tumba wa Tanzania One Theatre (TOT) Salum Chakuku 'Kuku Tumba'. 

MTANDAO huu ulimtafuta Ngonyani kupata ukweli wa taarifa hizo ambapo alikiri kuteta na Choki na kusema kila kitu kitawekwa wazi mambo yatakapoiva. Kwa upande wake Choki alisema,aliitwa na mfanyabiashara huyo kutoa ushauri wa namna ya kuiboresha bendi hiyo ila hafahamu habari za kuondoka Twanga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...