Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani
akiwasalimia wachezaji wa Karakana City wakati akikagua timu za mchezo
wa Nage zilizoingia Fainali ya Mashindano ya Nage Mapinduzi CUP
2016-2017. Aliyevaa kofia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, ambaye ndiyo
mwandaaji wa Mashindano hayo. Ngonyani aliyafunga Mashindano hayo
yaliyofanyika katika Uwanja wa Amani, mjini Unguja, Zanzibar.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani
akizungumza na mamia ya wananchi waliouhudhuria katika Fainali ya
Mashindano ya Nage Mapinduzi CUP katika Uwanja wa Amani, mjini Unguja,
Zanzibar. Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, ambaye ndiyo
mwandaaji wa Mashindano hayo. Ngonyani aliyafunga Mashindano hayo
yaliyofanyika katika Uwanja wa Amani, mjini Unguja, Zanzibar. Kulia ni
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.
Hamisi Kigwangala. Katika mashindano hayo, timu ya Six Centre iliibuka
mshindi dhidi ya timu ya Karakana City zote za mjini Unguja. Picha na
Felix Mwagara.
Mbunge
wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani
(wapili kulia) kuja kufunga Fainali ya Mashindano ya Nage Mapinduzi CUP
2016-2017 katika Uwanja wa Amani, mjini Unguja, Zanzibar. Katika hotuba
yake Masauni ambaye ndiyo aliyeandaa msahindano hayo alisema, mchezo
huo utazidi kuthaminiwa ili kuwaweka vijana pamoja. Picha na Felix
Mwagara.
Mchezaji
wa timu ya Six Centre ya Mwera ambayo imepata ushindi, akikwepa mpira
katika mchezo wa Fainali ya Mashindano ya Nage Mapinduzi CUP 2016-2017,
kati ya timu hiyo na Karakana City ya Chumbuni, katika viwanja vya
Amani, mjini Unguja, Zanzibar. Picha na Felix Mwagara.
Msanii
wa kizazi kipya, Kheri Sameer Rajab (Mr. Blue), akitoa burudani huku
akishangiliwa na Waheshimiwa Wabunge pamoja na Wawakilishi wakati wa
Fainali za Mashindano ya Nage Mapinduzi CUP 2016-2017 yaliyofanyika
katika Uwanja wa Amani, mjini Unguja, Zanzibar. , Watatu kushoto ni
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akifuatiwa na Naibu Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangala. Picha na Felix Mwagara.
Mbunge
wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwa katika picha ya pozi na Msanii wa
nyimbo za Singeli, Manfongo kabla ya msanii huyo kupanda jukwaa kutoa
burudani katika
Mbunge
wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, (watatu kushoto), akiwa katika picha ya
pamoja na wasanii maarufu wa kizazi kipya kutoka Tanzania Bara na
Visiwani kabla ya Wasanii hao kupanda jukwaani kutoa burudani katika
Fainali ya Mashindano ya Nage Mapinduzi CUP 2016-2017 yaliyofanyika
katika Uwanja wa Amani, mjini Unguja, Zanzibar. Mashindano hayo
yaliandaliwa na Mhandisi Masauni ili kukuza vipaji vya vijana. Picha
zote na Felix Mwagara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...