Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Styden Rwebangila (wa kwanza kulia) pamoja na wataalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini wakiwa katika kivuko cha kuelekea katika Wilaya ya Ukerewe, Mwanza kwa ajili ya kukagua miradi ya umeme jua inayotekelezwa na kampuni ya Rex Energy.
Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Styden Rwebangila (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji kutoka kampuni ya Rex Energy, Francis Kibhisa (kulia) katika ziara hiyo.
Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Styden Rwebangila (kulia nyuma) pamoja na wajumbe wengine wakielekea katika kisiwa kidogo cha Ghana/Siza kwa ajili ya kukagua miradi ya umeme jua inayotekelezwa na kampuni ya Rex Energy.
Mkurugenzi Mtendaji kutoka kampuni ya Rex Energy, Francis Kibhisa (kulia) akielezea hatua ya utekelezaji ya miradi ya kusambaza umeme katika kisiwa cha Ghana/Siza wilayani Ukerewe kwa Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Styden Rwebangila (kushoto).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...