*Wasomi wamshukia, wamtaka aache siasa
WADAU mbalimbali wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwa muwazi kwa wananchi wake wakati wanapohitaji misaada mbalimbali wakati wa majanga.
Wametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hizi kueleza kauli ya hivi karibuni ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye amekaririwa akidai kuwa kauli za Rais mkoani Kagera ni za hatari.
Wamesema kuwa baadhi ya Watanzania wamezoea kupewa ahadi ambazo kwa wakati mwingine ni vigumu kutekelezeka na sasa watu kama Mbowe bado wako kwenye mtazamo huo.Wameongeza kuwa Rais Magufuli amekuwa siku zote mkweli, jambo ambalo baadhi ya watu wasiopenda ukweli wanapotosha kauli zake kwa kutaka kuwachonganisha wananchi na Rais wao ambaye amekusudia kuwaletea wananchi maendeleo.
Rais Magufuli akiwa Kagera hivi karibuni alisisitizia msimamo ambao si mpya, umekuwa msimamo wake na wa Serikali tangu yalipotokea maafa ya tetemeko la ardhi mkoani humo kwamba Serikali itasaidia lakini haitaweza kumjengea nyumba kila mtu.“Baadhi ya wanasiasa na viongozi wamekuwa wakitoa kauli zenye kupotosha na kubeza hotuba ya Rais Magufuli mkoani Kagera jambo ambalo sio zuri na sio ukomavu wa kiasa” walisema.
Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cvha Dar es Salaam, Dkt Bashiru Ally amesema kuwa katika mfumo wa siasa huru kuna kutofautiana mitazamo kati ya wananchi ,Serikali na viongozi wa siasa lakini ni wazi kuwa Rais alisimama katika msimamo wa Serikali yake na uwezo wa kutekeleza ahadi zake.
Alisema kuwa Rais Magufuli alikuwa na maana nzuri ya kukabiliana na majanga nchini inategemea uwezo wa nchi na mshikamano wa wananchi na huo ni ukweli ambao wengi hawakupenda kuusikia.
Dkt. Bashiru Ally alisema kuwa kwa janga la Kagera kulikuwepo mshikamano wa Serikali katika ngazi zote, wananchi na wadau mbalimbali walishiriki kwa namna moja ama nyingine kukabiliana na janga hilo.
“Wito wangu ni kuwataka wanasisa kujifunza kutokana na majanga badala ya kutoa kauli tatanishi na zenye kubomoa mshikamano wa wananchi, bali wanatakiwa kukosoa bila kubeza, kupotosha kwa namna ni ya kungwana,” alisema Dkt Bashiru
Kwa upande wake Dkt. Benson Bana kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema kuwa watu wanatafsiri vibaya maneno ya Mhe. Rais aliyoyaongea Mkoani Kagera hivi juzi.“Mheshimiwa ameongea ukweli kwa sababu ni sahihi kuwasaidia watu wengi kwa pamoja kuliko kumsaidia mtu mmoja mmoja,” alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...