Mkuu wa jeshi la taifa la Gambia, Jenerali Ousman Badjie ametangaza kumuunga mkono rais wa taifa hilo Yahya Jammeh licha ya mgogoro unaondelea nchini humo, kufuatia matokea ya Uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.

Rais Jammeh alishindwa katika uchaguzi mkuu wa urais wa nchi hiyo na mpinzania Adama Barrow. Awali alikubali matokeo ya uchaguzi huo lakini alibadili uamuzi siku kadhaa baadaye akitaja kuwepo kwa udanganyifu wa matokeo ya kura katika uchaguzi huo.

Katika taarifa iliyotolewa na magazeti yanayounga mkono serikali, Jenerali Ousman Badjie aliahidi kwamba jeshi litaendelea kumtii rais huyo ambaye bado yuko madarakani sasa.

Uingiliaji wa kati wa Jenerali Badjie unafuatia vitisho vya kijeshi vya jamii ya kiuchumi ya mataifa ya Magharibi ECOWAS iwapo Jammeh atakataa kuondoka madarakani ifikiapo Januari 19.

Rais Jammeh amesema kuwa hatua yoyote kama hiyo itasababisha vita.

Kundi la bwana Barrow awali lilikuwa limedai kuungwa mkono na Jenerali Badjie.
Hatua hiyo ya Jeshi inaonekana kuleta utata katika kuanzisha serikai mpya baada ya Jammeh iliyokuwa madarakani kwa miaka 22.

Taifa hilo dogo la Afrika magharibi halijawahi kuwa na ukabidhi wa mamlaka kutoka uongozi mmoja hadi mwengine kwa njia ya amani tangu taifa hilo lijipatie Uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka 1965.

Mzozo kuhusiana na matokeo ya uchaguzi umesababisha wasiwasi, huku mataifa jirani na jamii ya kimataifa yakimtaka rais Jammeh kuondoka mamlakani. chanzo: BBC Swahili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...