Mwanamuziki maarufu nchini Marekani na Duniani kwa ujumla, Janet Jackson amejifungua mtoto wa kwanza (mtoto wa kiume) akiwa na umri wa miaka 50.
Taarifa hiyo iliyothibitishwa na afisa wake wa mawasiliano imesema mwanamuziki huyo na mumewe Wissam Al Mana, ambaye ni mfanyabiashara kutoka Qatar, wana furaha kumpata mtoto wa kiume ambaye wamempa jina la Eissa Al Mana.
"Janet alijifungua bila matatizo yoyote na kwa sasa anapumzika," alisema afisa wake huyo.
Janet Jackson ndiye mwanamke maarufu wa pekee aliyejifungua mtoto akiwa na umri mkubwa, wakati Mshindi wa tuzo ya Oscar, Halle Berry alijifungua mtoto wake wa pili akiwa na miaka 47 miaka mitatu iliyopita, wakati mke wa Mcheza filamu John Travolta, Kelly Preston, alijifungua mtoto wake wa tatu akiwa na miaka 48. ambapo huko nchini India nako kuna wanawake watatu ambao wamedaiwa kujifungua watoto wakiwa na umri wa zaidi ya miaka 70.
Janet Jackson na hazbendi wake Wissam Al Mana waliponaswa wakipiga misele katika mitaa ya Jiji la London, Nchini Uingeleza, miezi michache iliyopita.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...