Katibu
wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa Baraza la
Michezo Zanzibar Ndg Khamis Said akimfariji Mume wa Marehemu Amina
Athumani Ndg Toufik Majaliwa alipofika nyumbani kwa jamaa wa marehemu
katika mtaa wa kariakoo unguja leo. kutowa mkono wa pole akiwa na
waandishi wa habari za michezo Zanzibar ZASWA.
Kwa
taarifa za msemaji wa familia Ndg Nurdin Ramadhani amesema mwili wa
marehemu tasafirishwa kesho asubuhi na Boti ya Kampuni ya Azam Marine
saa moja asubuhi kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Kijiji kwao
Lushoto siku ya Jumanne mchana.
Mwili
wa marehemu utawasili jijini Dar es Salaam saa tatu asubuhi ukitokea
Zanzibar baada ya kuwasili katika bandari ya Dar es Salaam utasafirishwa
kuelekea kijiji kwao Wilaya ya Lushoto Mkoano Tanga kwa ajili ya
mazishi.
Katibu
wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar Ndg Khamis Said akizungumza na
waandishi wa habari za michezo Zanzibar Zaswa alipofika nyumbani kwa
ndugu wa marehemu katika mtaa wa kariakoo zanzibar.
Mwenyekiti
wa Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo Zanzibar Ndg Mwinyimvua
Mnzuki akizungumza na waandishi wa habari kwa kupokea kwa masikitiko
kifo cha mwandishi mwezao mrehemu amani athuman kilichotokea leo asubuhi
katika hopspitali ya mnazi mmoja.
Ndugu wa marehemu wakiwa msibari wakisubiri taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea Wilayani Lushoto Mkoani Tanga.
Wanafamilia wa marehemu Amina Athumani wakiwa katika msiba huo katika mtaa wa kariakoo Zanzibar.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot
Zanzinews.com.
0777424152 Or 0715424152.,
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...