Image may contain: 6 people, people smiling, crowd and outdoor
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mh.Amos Makala leo amekagua ukamilishaji wa madarasa kwa wanafunzi 406 waliokuwa wamekwama kuanza masomo kutokana na upungufu wa Madarasa.

Kati ya wanafunzi 406 waliokosa nafasi kuanza masomo ni 192,madarasa yao yamekamilika na wanafunzi 214 madarasa yao yatakamilika ndani ya siku 14.


"Hivyo ili wanafunzi 214 wasiendelee kuchelewa kuanza masomo yao,nimeagiza kuwa maabara ambazo zipo na hazijaanza kutumika kwa kukosa Vifaa, sasa zitumike kama madarasa kuanzia kesho Jumatatu, na baada ya madarasa kukamilika Januari 30 2017,Wanafunzi hao watatumia madarasa hayo",alisema Mh.Makala.


Rc.Makala amezipongeza halmashauri za jiji la Mbeya na Mbeya vijijini kwa kuchangia ukamilishaji wa madarasa na amewashukuru wananchi na wadau kwa kuchangia ujenzi wa madarasa.Habari Picha na Mr Pendo-MMG.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...