Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (katikati) akizungumza na vikundi vya wanawake na vijana kutoka katika Jiji la Arusha kabla ya Kukabidhi hundi za Mikopo ya robo ya kwanza na ya Pili kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.

Nteghenjwa Hosseah, Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amefungua mafunzo ya ujasiriamali kwa vikundi vinavyokopeshwa na kutoa mikopo kwa vikundi 85 vya wanawake na vikundi 40 vya vijana kutoka katika kata zote za Jiji la Arusha.

Akikabidhi hundi zenye thamani ya Sh Mil 624 kwa vikundi hivyo ikiwa ni mikopo ya robo ya kwanza na ya pili kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Mhe. Gambo amewataka kinamama na vijana kutumia fedha hizo kwa shughuli zilizokusudiwa ili ziweze kuleta manufaa na kuwatoa katika lindi la umasikini.

 “Mikopo hii inatolewa ili kuendeleza shughuli za kijasiriamali ambazo ndizo zilizopelekea mkidhi vigezo vya kupata Fedha; Nimatumaini yangu fedha hizi zitawawezesha kuongeza mitaji yenu na kuwapa ari ya kujituma zaidi huku mkizingatia nidhamu ya pesa ili muweze kuzirejesha kwa wakati na makundi mengine waweze kupata fedha hizo”Alisema Rc Gambo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(Katikati) akikabidhi hundi ya Tsh Mil 425 kwa wawakilishi wa Wanawake Bi. Mariamu Okash(Kata ya Kati) na Rose Charles(Kata ya Olorieni).

Aliongeza kuwa tofauti na mikopo hii ya halmashauri baada ya kuwawezesha vijana waendesha boda boda kwa kuwapatia Pikipiki 200 kundi litakalofuata ni wakinamama ambao watanufaika na Fedha zitakazorejeshwa na vijana hao kwa kupewa mitaji midogomidogo kadiri ya uhitaji.

Aidha Rc Gambo alimuagiza Mkurugenzi wa Jiji kuunda timu maalumu ya kuchunguza utoaji wa Mikopo kwa Kipindi cha Miaka mitatu kama ilifuata taratibu, vikundi vilivyonufaika kama ni hai  na hali ya urejeshaji.

Naye Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Kalisti Lazaro Bukhay ambaye alishiriki katika zoezi  la utoaji mafunzo na kukabidhi hundi amesema Kikundi ambacho hakitarejesha fedha zote za mkopo ama kuchelewesha marejesho kwa namna yeyote ile hakitapatiwa mkopo katika mwaka unaofuata ila wale watakaofanya vizuri katika biashara zao na kukuza mitaji wataongezewa kiasi cha kukopa kulingana na hali ya shughuli zao.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo akikabidhi hundi ya Tsh Mil 199 kwa wawakilishi wa Vijana Amos Kosani (Daraja II) na Janeth Prosper (Kata ya Unga Ltd).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...