NA HAMZA TEMBA - WMU
Serikali
kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema italipa madeni yote ya miaka ya
nyuma ya vifuta jasho na vifuta machozi ambayo inadaiwa na wananchi waliokubwa
na vitendo vya uharibifu wa wanyamapori nchini kabla ya bunge lijalo la
bajeti, madeni hayo ni yale ambayo yameshaifikia wizara hiyo na
kuhakikiwa.
Akizungumza
jana na uongozi wa wilaya ya Bunda wakati wa kuhitimisha ziara yake ya siku
moja ya kufuatilia changamoto za uhifadhi wilayani humo, Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Makani amesema uamuzi huo wa Serikali
utaondoa kilio cha muda mrefu cha wananchi ambao wamepata madhara mbalimbali ya
wanyamapori ikiwemo vifo, majeruhi, kuliwa mazao na kuharibiwa mashamba
yao.
"Serikali
ya awamu ya tano imeshakamilisha takwimu za madai, yale yote tunayodaiwa huko
nyuma, yaliyoifikia Wizara yakafanyiwa uhakiki na nimesema kwenye uhakiki huo
ndani ya kipindi cha miaka kumi, kwa wilaya zaidi kidogo ya 80 ambazo ndizo
zina changamoto hizi kwa kiwango kikuu, deni jumla ni shilingi 2,081,532,700
(bil. 2.9)", amesema.
Amesema
wilaya ambazo zimeathirika zaidi na vitendo hivyo na ambazo madai yao ni
makubwa zaidi ya Wilaya zingine ni Serengeti na Bunda ambazo ziko mkoani Mara
na zinapakana na Hifadhi ya taifa ya Serengeti, Ziwa Victoria, Pori la Akiba
Grumeti na Ikorongo. "Serengeti ndiyo inayoongooza kwa madai hayo,
shilingi milioni 408,547,600 alafu Bunda shilingi milioni
265,969,750",.
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akikagua moja ya shamba la mahindi lililoharibiwa na tembo katika kijiji cha Kunzugu, wilaya ya Bunda Mkoani Mara jana wakati wa ziara yake ya kuangalia changamoto za uhifadhi mkoani humo. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili.
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa pili kulia) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kunzugu, wilaya ya Bunda, mkoani Mara jana alipotembelea moja ya shamba la mahindi lilioharibiwa na tembo wakati wa ziara yake ya kuangalia changamoto za uhifadhi mkoani humo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...