Na Amina Kibwana-Globu ya Jamii.
 
Wizara ya ardhi,nyumba na maendeleo ya Makazi kupitia idara ya nyumba imepewa jukumu la kusimamia mfuko wa mikopo ya Nyumba kwa watumishi wa serikari kwa lengo la kuwawezesha watumishi wake kujenga,kununua au kukarabati nyumba kupitia mkopo huo mwenye masharti nafuu.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Idara ya nyumba Michael Mwalukasa amesema kuwa mfuko huu ulianzishwa kwa ajili ya kusaidia na kuwawawwzesha watumishi wa serikali wanaoishi mjini na vijijini kupata mkopo wa nyumba wenye masharti nafuu kwa ajili ya kujenga au kununua nyumba.

Ameongeza kuwa mfuko huo unatoa mikopo kuanzia milioni 20 kwa riba ya asilimia tatu ambao muda wa juu wa kurejesha mkopo huo ni miaka thelasini(30) katika kipindi cha utumishi kabla ya kustaafu au anapoacha utumishi kwa sababu zozote zile.

Mwalusaka amesema kuwa kuna sifa mbalimbali  za kupata mkopo huu ikiwa ni pamoja na mkopaji ni lazima awe mtumishi wa serikali, raia wa Tanzania,aliyeajiriwa kwa masharti ya kudumu na kuthibitishwa kazini pamoja na kuwa na hati ya kiwanja ambacho kitamuwezesha kupata mkopo kwa ajili ya kujenga.

Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi mikopo ya nyumba Lucy Kabyemera ameeleza faida za mikopo hiyo kwa watumishi wa  serikali ikiwa ni pamoja na kuwawezesha watumishi kupata mikopp yenye riba nafuu, kuweza kumiliki nyumba kwenye maeneo yenye hadhi,kuchochea kasi ya maendeleo kwenye miji na wilaya mbalimbali pamoja na kutoa fursa kwa watumishi kumiliki nyumba kwa kadri ya matakwa yao.

"Faida zipo nyingi sana kwani pamoja na kunufaika na mikopo baadhi ya wakopaji pia wameendelea kunufaika na ushauri wa kutumia technologia ya bei nafuu ya ujenzi kutokana na tafiti zilizofanywa na taasisi iliyopo chini ya Wizara (NHBRA)."

Kabyemera ameongeza kwa kusema kuwa ujenzi wa nyumba unahitaji gharama nyingi hivyo ndio maana wameamua kutoa mikopo hasa kwa watumishi wa serikali ili iweze kuwasaidia kwa kuwapa fedha taslimu ya shilingi milioni 20.

Mfuko wa Mikopo ya Nyumba ni moja wapo ya vyombo vilivyoanzishwa na serikali mara baada ya nchi kupata uhuru mnamo mwaka 1963 kupitia waraka wa watumishi wa serikali na.8 na badae kuendeshwa kupitia waraka wa watumishi wa serikali na.4 wa mwaka 1965.
Mkurugenzi wa Idara ya Nyumba Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Michael Mwalukasa akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam kuhusu mfuko wa kuwawezesha watumishi wa Serikali kumiliki Nyumba ambapo zaidi ya watumishi 2000 wameshanufaika na mikopo yenye riba nafuu ya asilimia 3 ili kuwawezesha kumiliki nyumba bora. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Mikopo ya Nyumba Bi Lucy Kabyemera na Kushoto
Mkurugenzi Msaidizi Mikopo ya Nyumba,Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Lucy Kabyemera akifafanua kwa waandishi wa habari kuhusu faida wanazopata watumishi wa Umma kutokana na mikopo inayotolewa na Serikali ili kuwawezesha kumiliki makazi bora. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Nyumba Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Michael Mwalukasa.Picha na Frank Mvungi-Maelezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...