Kamati ya Mpito TZUK kwa masikitiko makubwa imepokea taarifa za msiba wa baba mzazi wa Ndugu yetu na mwanajumuiya mwenzetu Chris Lukosi, Marehemu Mzee BONIFACE PANGAWE LUKOSI ambaye amefariki juzi  tarehe 3/01/2017, nyumbani Tanzania.

Taratibu za msiba zinaendelea kufanywa na watoto wa marehemu hapa U.K. wanatazamia kusafiri kesho alfajiri kuelekea Tanzania.Tunaomba kuwaombea safari njema na Mungu awape Faraja katika kipindi hiki kigumu. Wanajumuiya, Watanzania, Ndugu, Jamaa, na marafiki tunawaomba sana tujitoe kwa hali na mali kuwafariji watoto wa marehemu katika kipindi hiki kigumu na cha majonzi.

Michango yote ielekezwe moja kwa moja 

kwa mtoto wa marehemu Ndugu Chris Lukosi kupitia;

Account name - Chris Lukosi

Account No. 47710160

Sort Code.  60-17-31

Natwest Bank

Kamati ya Mpito TZUK Itaendelea kuwapa taarifa zaidi za msiba na mahitaji nyumbani Tanzania, Mungu awabariki kwa kujitoa kwenu kuwafariji na kuwa pamoja na familia ya Marehemu πŸ™πŸΎπŸ™πŸΎ

UPDATES:

Mfiwa Chris Lukosi na dada yake mkubwa (pichani kushoto) wamewasili jijini Dar es salaam kwa ndege ya Swissair kutoka Uingereza usiku wa kuamkia leo. Baada ya kuwasili wameenda nyumbani Yombo Vituka jirani na Malawi Hospital. Kufika huko unapita njia ya Jet Club, kituo cha kwanza cha basi unaulizia na kuoneshwa msibani ambako kunaangaliana na hiyo hospitali. 
LATEST UPDATES:
Misa ya kumuaga  Marehemu Mzee Lukosi itafanyika kesho IJUMAA saa nane mchana kwenye kanisa la Mtakatifu Yohana lililopo Yombo Vituka mwisho wa Lami. Baada ya misa safari ya kusafirisha mwili kuelekea Kalenga, Iringa, kwenye mazishi itaanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...