Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, amepuuzilia mbali madai ya Korea Kaskazini kuwa imeunda Kombora linaloweza kuwasilisha zana za nyuklia hadi Marekani.

Katika mawasiliano kupitia mtandao wa Twitter, Trump aligusia majigambo ya kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, katika ujumbe wake wa mwaka mpya ambapo alisema kuwa maandalizi ya kombora la aina hiyo yamefikia hatua ya mwisho.

Trump alisema katika ujumbe wake kuwa "Haitawezekana." Tamko lake la haiwezekani, halikueleweka vizuri kwa sababu wachanganuzi hawajui iwapo alimaanisha kuwa Korea Kaskazini haina uwezo huo au alikuwa akiandaa hatua ya kujikinga.
Trump pia alishutumu Uchina kwa kushindwa kumdhibiti mshirika wake Korea Kaskazini na pia akailaumu Beijing kwa kupokea pesa kiasi kikubwa cha pesa na mali kutoka Marekani. CHANZO: BBC SWAHILI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...