Mhe Charles Mwijage, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji asisitiza mageuzi ya kiuchumi kwa maendeleo ya watu yanayolenga katika kujenga viwanda na kupunguza biashara ya kuuza malighafi na ilenge kwenye kuhamasisha biashara za kuuza bidhaa zilizoongezwa thamani. 

Hayo aliyasema kwenye uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maendelo ya Biashara Tanzania (TanTrade) uliofanyika tarehe 16 Januari, 2017 katika ofisi za TanTrade zilizopo kwenye kiwanja cha Mwl J.K Nyerere barabara ya Kilwa. 

Mhe Mwijage amesema kuwa kazi kubwa ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ni kuhamasisha shughuli za biashara Tanzania na wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji ni wizara ambayo matumaini mengi ya watanzania yameangalia huko hivyo watu wanategemea matumaini makubwa sana. 

Akaendelea kwa kusema kuwa kwa mwaka 2017 kwenye maonesho ya 41 ya kimataifa ya biashara ya Dar es Salaam (DITF) yawe ya tofauti kwa watakaokuja kuonyesha bidhaa zao kutoka nchi za nje, waoneshaji hao waje na mashine za viwanda vidogo ili watanzania watakaokuja kuona na kununua mashine hizo ziweze kusaidia kuongeza thamani za bidhaa zao ili kasi ya kuuza malighafi nje ya nchi ipungue bali bidhaa za viwandani ziweze kuongezewa thamani ili kuweza kuuza nje ya nchi. 

Mhe Mwijage aliendelea kuiambia Bodi ya Wakurugenzi iliyoteuliwa kuwa kazi zote ambazo zilisimama zifanyiwe kazi mapema ili kueza kukamilisha maamuzi yote usiku na mchana akaongeza kwa kusema kuwa maamuzi ambayo hayakufanyika ni mabaya mno na gharama zake ni kubwa afadhali maamuzi ambayo yamefanyika ila mabaya hivyo asingependa kufanya maamuzi ya bodi bila bodi kumshauri ili aweze kufanya kazi yake kwa ufanisi. 
Mhe Charles Mwijage akimkabidhi vitendea kazi Mhandisi Christopher Chiza Mwenyekiti mpya wa bodi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Tanzania baada ya uzinduzi wa bodi hiyo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...