Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt.Augustine Mahiga
anatarajia kumpokea Waziri wa mambo ya nje wa Jamuhuri ya watu wa china
Mh.Wang Yi anayetarajia kufanya ziara ya kikazi nchini Tanzania Januari 9 Kwa lengo la kukuza mahusiano mazuri baina ya china na
Tanzania na kuangalia maeneo mapya ya ushirikiano wa kiuchumi.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam msemaji wa Wizara ya mambo
ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga amesema kuwa
wakati wa ziara hiyo Waziri Wang Yi atakutana na Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Mh Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na
kufanya mazungumzo na Dkt Mahiga kuhusu masuala mbalimbali ya
ushirikiano wa Kimataifa baina ya Tanzania na China.
"Kwakuwa
china iliichagua Tanzania kuwa miongoni mwa nchi nne barani Afrika
zitakazo wezeshwa kupiga hatua kwenye maendeleo ya viwanda hivyo kupitia
mpango huo tunatarajia viwanda takruban 200 vitajengwa au kuwekezwa
nchini."
Amesema kuwa mbali na
uendeshaji wa viwanda viongozi hawa watazungumzia miradi mingine ya
miundombinu ambapo china imeahidi kuisaidia Tanzania ikiwa ni pamoja na
maboresho makubwa ya Reli ya Tazara, Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo
pamoja na ujenzi wa Reli ya Kati.
Aidha Mh. Yi
anatarajiwa kuzungumza na mwenyeji wake kuhusu masuala ya ushirikiano wa
Kimataifa ikiwa ni pamoja mageuzi ya Baraza la usalama la Umoja wa
Mataifa ambapo china inaunga mkono msimamo wa Afrika na wa Tanzania
kutaka Afrika ipewe viti viwili vya kudumu kwenye barala hilo na kepewa
kura ya turufu, Masuala ya amani na usalama katika eneo la Afrika
Mashariki pamoja na eneo la Bahari ya kusini mwa china.
Ameongeza
kuwa mpango huo unaenda sambamba na mpango wa Taifa wa maendeleo wa
mwaka 2016/2020 kupitia ahadi za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania,Mh.John Pombe Joseph Magufuli wa kujenga Tanzania ya viwanda
ifikapo mwaka 2020.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...