Na Woinde Shizza,Arusha

Jumla ya shilingi  4,708,680,000 zimekusanya na jeshi la polisi mkoa wa Arusha kikosi cha usalama barabarani kutokana na faini zilizolipwa na watumiaji wa vyombo vya  moto  kwa kipindi cha January 2016 hadi December 2016 hiii ikiwa ni ongezeko kubwa tofauti na miaka iliopita

Hayo yamebainishwa na kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Charles   Mkumbo wakati akiongea na waandishi wa habari  kwa ajili ya kutoa taarifa ya hali ya usalama kwa kipindi chote cha mwaka 2016 kuanzia Januari hadi Disemba  ambapo alisema kuwa kwa upande wa ukusanyaji wa notification  fedha zimeongezeka kwa kiasi kikubwa.

Alisema kuwa  tozo hizo za notificationi katika kipindi cha mwaka 2016 ziliongezeka hadi kufikia shilingi 4,708,680,000/=  tofauti na mwaka 2015 ambapo jumla ya shilingi 3,227,640,00/= zilikusanywa kwa  hivyo kutokana na takwimu hizo kikosi cha usalama barabarani kimekusanya ongezeko la zaidi ya shilingi 1,481,040,000/=.

“fedha hizi zimeongezeka kutokana na makosa mbalimbali yanayofanywa na madereva mbalimbali wa vyombo vya moto kwa kujua wanavunja sheria ,na wengine wakiwa wanafanya kwa kutokujua sasa sisi kama jeshi la polisi tunatumia njia ya kuwaonya kwa kuwatoza faini ili waweze kujirekebisha  kwa haraka kwa sababu tusipo fanya hivyo na kuwaonya bila kuwapiga faini watakuwa wanarudia makosa kila siku ,na pia ongezeko hilo limetokana na kuwepo na ongezeko kubwa la watu wanaotumia vyombo vya moto ,mfano ukiangalia  magari mjini uwezi kufananisha magari yaliyokuwepo mwaka jana na mwaka huu mwaka huu yameongezeka kwa kasi na hata pikipiki pia ni hivyo hivyo”alisema Mkumbo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera Police Arusha, kazi nzuri sana ya ukusanyaji mapato. Ongezeko la asilimia 32 (32%)ni hatua nzuri ya kuukaribisha mwaka mpya.
    Makosa barabarani yapo mengi sana, kwa sababu hiyo basi pesa nyingi zinapotea aidha kwa kuingia kwenye mifuko binafsi au kwa kuwa na miundo mbinu finyu ya kusaidia kukusanya haya mapato.Ili tuweze kukusanya mapato maradufu inatubidi tuwekeze kwenye technolojia mpya ya ukusanyaji mapato yanayotokana na barabara (road offenders' fines). Kwa mfano mdogo to ni jinsi gani madereva wasivyo heshimu kivuko cha miguu (pundamilia). Kama police watawinda maeneo kama haya watapata pesa nyingi sana. Kuweka CCTV cameras kwenye bize roads kwani madereva wengi hawana uvumilivu kwenye foleni hivyo wengi wao huvunja sheria za barabara kwa kisingizio cha nachelewa/ninaharaka. Nawaomba Police Arusha huu mwaka 2017 wajiwekee target ya 1 trilion so that usalama barabarani ukapewa kipaumbele. Hili zoezi linawezekana kama litafanyika KIUKWELI, HAKI na USAWA. Plani kama hizi zianzie ngazi ya serikali ya mtaa kwenda juu.
    Asanteni
    MT

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...