- Wateja kujishindia vifaa mbalimbali vya majumbani kupitia droo ya Bahati nasibu
·
Airtel na Tecno wawazawadia wateja wake wa Smartphone
Kampuni
ya mkononi ya Airtel Kwa kushirikiana na Tecno mobile leo imewazawadia
wateja wake kupitia promosheni iliyozinduliwa maalumu kwa msimu wa
sikukuu za crismass, mwaka mpaya
na valentine kwa lengo la kuwahamasisha wateja kutumia simu za kisasa
za smartphone na kujishindia
Promosheni
hiyo ilihusisha wateja wa Airtel wanaonunua simu aina ya TECNO N6 and
TECNO W3 kwa kipindi cha sikukuu za krismasi, mwaka mpya na valentine
na kisha kupata nafasi ya
kuingia kwenye droo ili kujishindia vifaa mbalimbali vya nyumbani
vikiwemo , Televisheni, Mashine ya kutengenezea Juisi, Jiko la kuchoma
nyama, Mashine ya kutengeneza Sandwich , Brenda mashine pamoja na simu
za smartphone za TECNO W4 mbili
Akiendesha
droo hiyo iliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya Airtel Morocco
Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema “Airtel tuefika
mwisho wa promosheni yetu lakini
bado smartphone zinapatikana katika maduka yetu zikiambatana na ofa
kabambe. Napenda kuwashukuru wote walijiunga na ulimwengu wa smartphone
kupitia promosheni hii nakuwaomba wateja wetu wengine waendelee
kutembelea maduka yetu ili kupata simu za kisasa kwa
bei nafuu na kufurahia huduma zetu bora ikiwemo, Airtel Money Relax,
huduma ya Inteneti na nyingine nyingi”
Kampuni
ya Airtel ilizindua promosheni ya shinda na Smartiphone mwishoni mwa
mwaka jana ili kila mteja wake anaenunua simu aweze kupata nafasi ya
kushinda.
Meneja
wa Tecno Mobile Tanzania, Marco Wang akisoma jina la mshindi wakati wa
kuendesha bahati simu ya jishindie Tecno smartphone kupitia promosheni
maalumu iliyoendeshwa na Airtel pamoja na Tecno wakati wa msimu wa
sikukuu ambapo mwisho wake ni leo na washindi 7 wamepatikana.
Akishuhudia (wakwanza kulia) ni Meneja Uhusiano wa Airtel Bwn Jackson
Mmbando, akifatiwa na msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha bwana
Bakari Majid , na kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma kwa wateja
, Bi Adriana Lyamba.
Afisa
huduma kwa wateja wa Airtel , Bwn Pascal Maziku Akiokota jina la
mshindi wakati wa kuendesha bahati simu ya jishindie Tecno smartphone
kupitia promosheni maalumu iliyoendeshwa na Airtel pamoja na Tecno
wakati wa msimu wa sikukuu ambapo mwisho wake ni leo na washindi 7
wamepatikana. Akishuhudia (wakwanza kulia) ni Meneja Uhusiano wa Airtel
Bwn Jackson Mmbando, akifatiwa na msimamizi wa bodi ya michezo ya
kubahatisha bwana Bakari Majid, na kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha
huduma kwa wateja , Bi Adriana Lyamba
Meneja
Uhusiano wa Airtel Bwn Jackson Mmbando akitangaza majina ya washindi wa
promosheni maalumu iliyozinduliwa wakati wa msimu wa sikukuu
inayowawezesha wateja wa Airtel kujishindia zawadi mbalimbali pindi
watakaponunua simu za smart phone za Airtel. Washindi 7 wamepatikana
katika droo ya Bahati nasibu iliyochezeshwa leo katika makao makuu ya
Airtel Morocco jijini Dar es saalam , akishuhudia kushoto ni Mkurugenzi
wa Kitengo cha huduma kwa wateja , Bi Adriana Lyamba
Mkurugenzi
wa Kitengo cha huduma kwa wateja , Bi Adriana Lyamba akionyesha simu
aina ya Tecno iliyokabithiwa kwa washindi wakati wa droo ya bahati
nasibu iliyochezeshwa katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar
es Saalam
Wafanyakazi wa Airtel na wafanyakazi wa Tecno wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kuchezesha droo ya bahati nasibu,
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...