MKE wa Rais Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wametembelea Gereza la Mahabusu Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu gerezani hapo. 
Wake wa viongozi wametembelea gereza hilo Jumanne, Februari 14, 2017wakiwa katika ziara mkoani Tabora, ambapo Mama Janeth amesema wameamua kuwatembelea wafungwa na mahabusu hao kwa nia ya kuwafariji kwa kuwa wao ni sehemu ya jamii. 
“Vitabu vitakatifu vinasema kwamba ukiwasaidia watu wenye mahitaji utakuwa umetoa sadaka kubwa kwa Mwenyezi Mungu, hivyo tumeamua kuja kutembelea wafungwa na mahabusi kwenye gereza hili na kuwapa zawadi kwa kuwa nanyi mnahitaji faraja,” amesema. 

Amesema wameamua kwenda kuwaona wafungwa na mahabusu hao kwa lengo la kuwafariji na kuwatia moyo kwa sababu wanaimani kwamba wakitoka watakuwa raia wema na hayo wanayopitia ni sehemu ya kufanya marekebisho ya tabia. 
“Ni siku kubwa kwangu, nimejifunza mengi baada ya kufika hapa. Kitendo cha kwenda kuwaona wenye mahitaji wakiwemo wagonjwa, wafungwa ni jambo jema tunaamini hizi zawadi tulizozitoa japo ni kidogo zitawasaidia kwa sababu tunajua mnamahitaji mengi,” amesema. 
Katika gereza hilo wake hao wa viongozi wamekabidhi zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu, ambapo mwakilishi wa wafungwa hao Deo Kitave aliwashukuru kwa niaba ya wenzake. “Tunawashukuru kwa kutukumbuka. Tunamuomba Mwenyezi Mungu muendelee kuwa na moyo huo,” alisema.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkabidhi zawadi  Naibu Mkuu wa gereza la Mahabusu Tabora Mrakibu wa Magereza Godliver Makwaruzi  wakati yeye na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu  Februari 14, 2017.
 Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa zawadi  Naibu Mkuu wa gereza la Mahabusu Tabora Mrakibu wa Magereza Godliver Makwaruzi  wakati yeye na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu  Februari 14, 2017
 Mke wa Rais Mama Janeth magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakitoka katika gereza la wanawake Tabora walipotembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu Februari 14, 2017

 Mke wa Rais Mama Janeth magufuli akiongea machache wakati yeye na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa  walipotembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu Februari 14, 2017
 Mke wa Rais Mama Janeth magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakitoa zawadi kwa ajili ya wafungwa na mahabusu walipotembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu  Februari 14, 2017
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...