Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Msafara wa mwanamuziki wa bongo fleva,
Ally Kiba jana alisimamisha jiji la Dar es Salaam kwa zaidi ya saa tatu
mara baada ya kuwasili kutokea nchini Afrika kusini
kuchukua tunzo yake ya Msanii bora barani Afrika.
Kiba ambaye aliwasili katika uwanja wa
kimataifa wa JNA majira ya saa nane mchana na kulakiwa na wapenzi lukuki ambao
aliambatana nao katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Msafara huo ambao ulianzia katika barabara
ya pugu kasha kuingia katika barabara ya Mandela na kuwapa fursa wakazi wa
buguruni na viunga vyake vya malapa na bungoni kushuhudia msanii huyo akiwa
katika gari ya wazi huku akionyesha tunzo yake huku wakazi hao wa
jiji wakimshangilia.
Kiba alipita katika eneo alilozaliwa la
Kariakoo mtaa wa Muheza na kumkabidhi mama yake tunzo hiyo na majirani zake
ambao walipiga shangwe ya kutosha kutokana na mafanikio ya msanii huyo.
Msafara wa msani huyo ulitoka kariakoo na
kupita katika mitaa ya Msimbazi, Upanga na barabra ya Sarenda kasha kuelekea
moja kwa moja katika hotel ya Double Tree Masaki kwa ajili ya mahojiano na
waandishi wa habari.
Ally Kiba akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere akitokea nchini Afrika Kusini mara baada ya kukabidhiwa tunzo yake ya MTV kama msanii bora wa kiume Afrika
Kiba kielekea kwenye gari maalum aliyoandaliwa mara baada ya kuzngumza na mashabiki wake
Ally Kiba akiwa na ndugu yake Abdul Kiba juu ya gari la wazi katika mita ya Buguruni
Ally Kiba akimkabidhi Tunzo yake Mama yake mzazi maarufu kama Mama k
Mama K ambaye ni mama mzazi wa Ally Kiba akionyesha Tunzo ya msani huyo juu. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...