Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki
ya Barclays Tanzania, Simon Mponji (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi
rasmi wa tawi la kisasa la benki hiyo katika jengo la Shirika la Nyumba (NHC),
mjini Morogoro mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji
wa Barclays Tanzania, Abdi Mohamed na kulia ni
Mjumbe wa Bodi ya benki hiyo, Dk. Suleman Mohamed.
Mkuu wa Mauzo wa Benki ya
Barclays Tanzania, (kushoto), akieleza kuhusu huduma mbalimbali za kibenki
zitolewazo katika tawi jipya Barclays la mjini Morogoro katika sherehe za
uzinduzi wa tawi hilo juzi. Wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji, Abdi
Mohamed, mjumbe wa bodi, Dk. Suleman Mohamed na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya
Benki ya Barclays, Simon Mponji .
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki
ya Barclays Tanzania, Simon Mponji (wa pili kulia), akizungumza na waandishi wa
habari katika hafla ya uzinduzi rasmi wa tawi jipya la benki hiyo mjini Morogoro. Wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Barclays, Abdi Mohamed na Mjumbe wa Bodi
ya benki hiyo, Dk. Suleman Mohamed.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...