Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia Mhe. Balozi Ombeni Sefue (wa pili kushoto) akipokea kompyuta kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Mhe. Song Geum Young, wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi na wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Diplomasia Dkt. Bernard Archiula.
Mhe. Balozi Sefue akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Bodi na Uongozi wa Chuo cha Diplomasia mara baada ya kupokea ufadhili huo kutoka kwa Serikali ya Jamhuri ya Korea.
Balozi Mwinyi akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambapo aliipongeza Serikali ya Jamhuri ya Korea kwa kuendelea kuwa mdau wa maendeleo katika sekta mbalimbali nchini hususan sekta ya Elimu.
Sehemu ya Wakufunzi wa Chuo cha Diplomasia wakimsikiliza Balozi Sefue (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa neno la shukrani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...