Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, tarehe 08 Februari, 2017 amefanya ziara ya
kushtukiza katika mradi wa ujenzi wa jengo jipya la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam (Terminal
3) na kuagiza shughuli za ujenzi wa uwanja huo ziendelee kuanzia kesho.
Awali Mkandarasi anayejenga uwanja
huo ambaye ni kampuni ya BAM International alitangaza kusitisha ujenzi kuanzia
leo kutokana na kutolipwa madai yake na Mhe. Rais Magufuli ameahidi kulipa
fedha hizo haraka.
Hata hivyo, Mhe. Rais Magufuli
ameelezea kusikitishwa kwake na namna mradi huo unavyotekelezwa ikiwemo Serikali
kukubali gharama kubwa za mradi ambazo ni Shilingi Bilioni 560 kiwango ambacho
ni kikubwa ikilinganishwa na jengo linalojengwa.
“Hivi kulikuwa na sababu gani za
nyinyi wataalamu wa Serikali kukubali gharama kubwa namna hii, hivi hili jengo
linafanana na Bilioni 560?
“Halafu mlikuwa na haraka gani
kuidhinisha kuanza awamu ya pili ya ujenzi kabla ya kumaliza awamu ya kwanza?” amehoji Mhe. Rais Magufuli
alipokuwa akiwauliza Wahandisi wa Wizara ya Ujenzi wanaosimamia ujenzi huo.
Kufuatia hali hiyo, Mhe. Rais
Magufuli amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame
Mbarawa Mnyaa aliyeongozana nae kuunda timu ya wataalamu watakaofanya tathimini
ya utekelezaji wa mradi huo ikiwa ni pamoja na kuzungumza na Mkandarasi anayejenga
uwanja huo na Mhandisi Mshauri ambao wamekubali kupunguza gharama za ujenzi wa
mradi huo.
“Serikali italipa fedha ambazo
Wakandarasi wanadai lakini, nataka Waziri uunde timu ya kufanya tathmini upya,
ni lazima hii gharama ipungue, hatuwezi kumaliza fedha zote hizi wakati jengo
halifanani na thamani hiyo” amesisitiza Dkt. Magufuli.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli ambaye
ameonesha kutofurahishwa na dosari zilizoanza kujitokeza katika baadhi ya
maeneo ya jengo hilo, amemuagiza Mhe. Waziri Mbarawa kuunda upya timu ya
Wahandisi watakaosimamia mradi huo na ambao watafanya kazi kwa uzalendo na
kusimamia ubora.
Kabla ya kuondoka uwanjani hapo
Mhe. Rais Magufuli amekutana na wafanyakazi walioajiriwa katika shughuli za
ujenzi wa uwanja huo na kuwahakikishia kuwa Serikali imechukua za kuhakikisha
mradi huo unaendelea na kwamba kuanzia kesho wataendelea na kazi kama kawaida.
Wakati
huo huo,
Mhe. Rais Magufuli amemsimamisha kazi Kaimu Katibu wa Tume ya Mipango (Wizara
ya Fedha) Bi. Frolence Mwanri aliyeidhinisha kuanza kwa awamu ya pili ya ujenzi
wa jengo hilo jipya la Uwanja wa Ndege kabla ya kumalizika kwa awamu ya kwanza
ili kupisha uchunguzi.
Mhe. Dkt. Magufuli ameviagiza
vyombo vinavyohusika kufanya uchunguzi katika mradi huo.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
IKULU
Dar es Salaam
08 Februari, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa
Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo Jumatano February
8, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege
wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo
Jumatano February 8, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege
wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo
Jumatano February 8, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege
wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo
Jumatano February 8, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na baadhi ya wahandisi na makadrasai alipofanya
ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Terminal III
kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo Jumatano February 8, 2017.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...