WATUMISHI katika Halmashauri ya
wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wameonywa kuacha kutumia vibaya fedha za
miradi zinazotokana na wafadhili kwenye maeneo yao kwani watakaobainika
kufanya hivyo watashughulikiwa ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo vya
sheria.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert
Gabriel wakati akipokea taarifa ya
umalizaji wa majengo ya matatu ya maabara yalijengwa na taasisi
isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha
ikishirikiana na A Better World kutoka Canada kwa shule ya sekondari ya
Patema iliyopo kata ya Mpale Wilayani humo.
Aidha wao kama viongozi wa serikali wilayani humo hawatakuwa na
mdhara
na watumishi ambao watabainika kuihujumu
miradi ya maendeleo inayopelekwa kwenye maeneo yao na wafadhili
mbalimbali kwani kufanya hivyo kunachangia kurudisha nyuma kasi ya
ukuaji wa maendeleo.
“Nisema wazi kuwa watumishi badilikeni kwani mimi kama kiongozi wa
wilaya hii sitamfumbia macho mtu yeyote
ambaye atakuwa kikwazo cha maendeleo kwenye wilaya hii na niwaonye wenye
tabia kama hiyo waiache mara moja.
Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga,Mhandisi Robert Gabriel akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Taasisi ya isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha Azidu Kaonekana wa pili kulia ambao wameshirikiana na A Better World kutoka Canada kufanya ujenzi wa majengo matatu ya maabara kwenye shule ya sekondari ya Patema iliyopo kata ya Mpale Wilayan
Kaimu Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Korogwe Vijijini,Martha Kusare kulia akipokea msaada wa sola ya mobisol kutoka kwa Mkurugenzi wa Taasisi isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha,Azidu Kaoneka ikishirikiana na A Better World kutoka Canada kwa shule ya sekondari ya Patema ili kuweza kutumia nishati ya umeme kwa ajili ya matumizi yao ambapo sola hiyo na ujenzi wa maabara tatu zilizojengwa na taasisi hiyo iligharimu kiasi cha sh.milioni 75
Mkurugenzi wa Taasisi isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha,Azidu Kaoneka akifuatilia maendeleo ya wanafunzi wa shule ya sekondari Patema wilayani korogwe Mkoani Tanga. HABARI ZAIDI BOFYA HAPA |
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...