Ecobank
Tanzania (ETZ) imezindua huduma mpya ya Ecobank Mobile App, hii ni njia
rahisi na ya haraka ya kibenki kupitia simu za mkononi. Ecobank Mobile
App itawawezesha wateja kufanya miamala mbalimbali ya kifedha ikiwemo
kuhamisha fedha - kote baina ya matawi na baina ya benki, kununua muda
wa maongezi, Malipo ya Ankara, kuangalia viwango vya kubadilisha fedha
za kigeni, maombi na kuangalia taarifa za benki, Malipo ya kibiashara,
pamoja na huduma za Kadi na hundi.
Zaidi, Ecobank Mobile App
itawawezesha wateja wa benki kuweza kuzifikia akaunti zao kupitia simu
za mkononi na chaneli USSD, hivyo kuwahakikishia unafuu, upatikanaji, na
kasi kwa saa 24 kwa juma huku ikiwaondolea ulazima wa kwenda au kupanga
foleni kwenye matawi ya benki hiyo ambayo kwa sasa yapo nane (8).
Tukio
hilo kwa sehemu kubwa lilihudhuriwa na halaiki ya watu ikiwa ni pamoja
na Bodi ya Wakurugenzi wa Ecobank, Wateja na Wafanyakazi wa benki,
Watendaji wa Kampuni ya Ecobank, Wanafunzi, Wanadiplomasia, Viongozi wa
Serikali, Wawakilishi kutoka Benki Kuu na washirika wa kibiashara wa
benki hiyo.
Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Ashatu Kijaji, alikuwa Mgeni Rasmi katika tukio hilo. Aliishukuru ETZ
kwa ubunifu huo ambao, alisema utaenda mbali sana katika kuharakisha na
kuimarisha juhudi za ushirikishwaji kifedha nchini Tanzania.
Aliipongeza
benki hiyo kwa kuunga mkono juhudi na kauli mbiu ya awamu ya tano ya
“Hapa kazi tu” kutokana na kuzindua bidhaa ambazo zimelenga
kuwarahisishia maisha watanzania.
“Badala ya watu kubeba fedha
mkononi sasa watabeba kidigitali” alisema na kuongeza kuwa utaratibu huu
sio salama tu bali ni rafiki kwa kuokoa muda hasa katika kipindi hiki
cha “Hapa kazi tu”.
Aliongeza kuwa Serikali itaendelea kuweka
mazingira wezeshi katika kuhakikisha benki zinafanya kazi kwa usalama na
kuunga mkono uchumi wa kutembea bila fedha taslim.
Naibu Waziri wa fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Ecobank Mobile App’ iliyozinduliwa jana jijini Dar es salaam. Programu hii ya kidijitali kutoka Ecobank ni mahususi kwa ajili ya kurahisisha huduma za kibenki kwa njia ya haraka na usalama kupitia simu za mkononi.
Naibu Waziri wa fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akipeana mkono na Kaimu Mwenyekiti wa bodi ya Ecobank Bw. Peter Machunde mara baada ya kuzindua rasmi huduma mpya ya kidijitali ya ‘Ecobank Mobile App’ iliyozinduliwa jana jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia (katikati) ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Ecobank-Afrika Bw. Ade Ayeyemi na Mkurugezi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Enoch Osei-Safo.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Ecobank wakifuatilia kwa makini hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya kidijitali ya ‘Ecobank Mobile App’ iliyozinduliwa jana jijini Dar es salaam. Programu hii ya kidijitali kutoka Ecobank ni mahususi kwa ajili yakurahisisha huduma za kibenki kwa njia ya haraka na usalama kupitia simu za mkononi.
Naibu Waziri wa fedha na Mipango Dr. Ashatu Kijaji akipakata maelezo kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wa Ecobank Tanzania kuhusiana huduma mbalimbali zinazopatikana kwenye programu ya kidijitali ya ‘Ecobank Mobile App’ iliyozinduliwa jana jijini Dar es salaam. Pamoja nae ni Kaimu Mwenyekiti wa bodi ya Ecobank Tanzania Bw. Peter Machunde.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...