Mkuu wa Wilaya ya Mufindi amewataka wananchi Wilayani Mufindi, kujenga utamaduni wa kupanda miti na kuacha tabia ya kuharibu miti na misitu kwa kuichoma moto na kuikata ovyo sanjari  na tabia ya kuishi ndani ya misitu kwani kwa kufanya hivyo ni kutenda kosa la jinai kwa mujibu wa sheria za misitu.

Tarifa ya kitengo cha habari na mawasiliano cha halmshauri ya Wilaya ya Mufindi, imebainisha kuwa, Mkuu huyo wa wilaya ameyasema hayo kupitia hotuba  iliyosomwa kwa niaba yake na katibu tawala wa Wilaya Bw. Aberdi Mwela wakati wa uzinduzi wa siku ya upandaji miti kiwilaya iliyofanyika kwenye eneo la Jeshi la Magereza katika kijiji cha Ikongosi juu Wilayani Mufindi.

Mkuu huyo wa Wilaya ameongeza kuwa, serikali iliamua kutunga  sheria hiyo baada ya kuona kumekuwa na uharibifu mkubwa wa misitu na mazingira tabia ambayo husababisha mabadiliko ya hali ya hewa , kuongezeka kwa hewa ya ukaa, kupungua kwa kiasi cha mvua na kubadilika kwa majira yake, kupungua kwa mazao mashambani pamoja na kuongezeka kwa joto duniani.

Aidha, ameongeza kuwa, siku ya upandaji miti nchini, inawakumbusha wakazi wote wa Mufindi, Mkoa wa Iringa na hata Taifa kwa ujumla wake, kuzingatia utunzaji wa miti, misitu na mazingira kwa kupunguza ukataji miti ovyo na kuongeza kasi ya upandaji miti ili kupunguza uharibifu wa mazingira kwani ukwasi tunaoweza kuwanao sanjari na uhai tulionao unategemea sana uwepo wa mazingira rafiki kwa mwanadamu na kuongeza kuwa viumbe vyote chini ya dunia vinategemea miti ili kuishi.

Halmahauri ya Wilaya ya Mufindi ni moja kati ya halmshauri zinazo shika nafasi za juu nchini kwa sifa ya kupanda miti ikiwa na misitu mikubwa huku baadhi ya vijiji vyake vikinufaika na mamilioni ya fedha kupitia  mradi wa kiduni wa kupambana na  hewa ukaa duniani.
katibu tawala wa Wilaya ya Mufindi Bw. Aberd Mwela akipanda mti wakati wa uzinduzi alipomwakilisha Mkuu wa Wilaya.
Wananchi wa kata ya Ikongosi wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza mgeni wa heshima na kushiriki upandaji miti uliokuwa ukifanyika katika shamba la Magereza kama sehemu teule ya uzinduzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...