Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro leo Jumamosi Februari 18,2017 amewaongoza wakazi wa Shinyanga kufanya mazoezi katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga. 

Mazoezi hayo yaliyoanza saa 12 asubuhi na kumalizika saa 2 asubuhi yamehudhuriwa pia na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini,Stephen Masele na Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro. 

Akizungumza wakati wa mazoezi hayo Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amesema wakazi wa Shinyanga wataendelea kufanya mazoezi kila siku Jumamosi ili kumuunga mkono Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan .
“Wiki iliyopita mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack alizindua mazoezi kimkoa,tumekubalina tuwe tunafanya mazoezi kila wiki siku ya Jumamosi ili kudhibiti Magonjwa yasiyo ya kuambukiza,nawakumbusha kuwa mazoezi ni afya hivyo wananchi naombeni muendelee kujitokeza kufanya mazoezi”,alisema Matiro. 

Hivi karibuni Makamu wa rais Samia Suluhu aliagiza amewaagiza viongozi wa mikoa na wilaya zote kuweka utaratibu wa kufanya mazoezi angalau kwa mwezi mara Moja.

Alisema kila Jumamosi ya pili ya mwezi itakuwa siku ya mazoezi ambapo aliwaasa wananchi kufanya mazoezi na kuanzisha na kujiunga na vikundi vya mazoezi na serikali itatimiza wajibu wake wa kuweka mazingira mazuri ya kufanyia mazoezi kote nchini.

Mwandishi wetu Kadama Malunde ametuletea picha 33 wakati wa mazoez hayo..Tazama hapa chini
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akitoa neno kwa washiriki wa mazoezi hayo ambapo alisema mazoezi ni afya na yanajenga upendo na kufahamiana kwa washiriki wa mazoezi
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Stephen Masele akizungumza na washiriki wa mazoezi hayo ambapo aliwahamasisha wananchi kuendelea kujitokeza kufanya mazoezi. 

Mratibu wa Mazoezi hayo,Diwani wa kata ya Kambarage Hassan Mwendapole akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ili azungumze na washiriki wa mazoezi hayo katika viwanja vya Shycom Mjini Shinyanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...