Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu. Kufuatia mapambano yanayoendelea nchi nzima dhidi ya watu wanaojihusisha na uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanya misako na Mafanikio yaliyopatikana katika Misako ni kama ifuatavyo:-
KUPATIKANA NA DAWA ZA KULEVYA [BHANGI].
Mnamo tarehe 11.02.2017 hadi tarehe 16.02.2017 kwa nyakati tofauti, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya misako dhidi ya watu wanaojihusisha na uuzaji, usafirishaji na matumizi ya dawa za kulevya. Katika misako hiyo iliyofanyika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya, watuhumiwa wanne walikamatwa wakiwa na dawa za kulevya aina ya Bhangi misokoto mitatu yenye uzito wa kilogram 15 na gram 685
Watuhumiwa waliokamatwa wakiwa na dawa za kulevya aina ya Bhangi ni:-
1. GEOFREY ADAMSON [35] Mkazi wa Mabatini
2. ZUBER MWAMBENYA [24] na 3. GWAKISA ANYOSISYE [20] wote wakazi wa Mama John na 4. PHILIBERT MOSES [35] Mkazi wa Nonde
5. MPOKI IBRAHIM [37] Mkazi wa Kitongoji cha Igogwe Wilaya ya Rungwe
6. AGUST KIHAULILO @ KIDEVU [63] Mkazi wa Igawa Wilaya ya Mbarali
7. CALVINS MOHAMED [25] Mkazi wa Ilemi.
8. NASSORO OMARI [17] Mkazi wa Mwambene
9. OTHMANI SAIDI [24] Mkazi wa Mwambene
10. KENEDY BROWN [21] Mkazi wa mwambene
KUTEKETEZA SHAMBA KUBWA LA BHANGI
Mnamo tarehe 16.02.2017 majira ya saa 16:20 jioni Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Kamati Kuu ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kipolisi Mbalizi lilifanya Oparesheni ya pamoja katika Kijiji cha Jojo kilichopo Kata ya Santilya, Tarafa ya Isangati, Wilaya ya Kipolisi Mbalizi, Mkoa wa Mbeya na kufanikiwa kumkamata UPE NDUTA [30] Mkazi wa Jojo akiwa amelima shamba la bhangi lenye ukubwa wa ekari moja.
Aidha katika Oparesheni hiyo zaidi ya miche 2,000 iliyokomaa ilikutwa shambani. Pia nyumbani kwake alikutwa na bhangi kilogram 2 na gram 145. Mtuhumiwa ni mkulima, muuzaji/msafirishaji na mtumiaji wa dawa za kulevya [Bhangi].
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...