Na Gasper Andrew- Singida.


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ameagiza maafisa mifugo kata kusimamia kwa karibu miradi ya ufugaji kuku na mbuzi inayotekelezwa na kaya maskini zilizopo kwenye mpango wa TASAF 111.

Amesema kuku au mbuzi katika miradi hiyo wakifa kwa kukosa huduma kutoka kwa maafisa mifugo,maafisa hao watalazimika kufidia kuku au mbuzi hao watakaokufa.

Akilijengea nguvu agizo lake hilo Dkt. Nchimbi alitoa kutoka mfukoni kwake shilingi 150,000 taslimu na kumpatia afisa mifugo kata ya Kikonge Wilayani Iramba kwa ajili ya kuikarabati pikipiki yake iweze kumrahihishia kufika kwenye miradi ya kaya maskini.

Dkt. Nchimbi ametoa agizo hilo juzi muda mfupi baada ya kumaliza kukagua bwawa la kijiji cha Kikonge wilaya ya Iramba linalojengwa kwa nguvu za kaya maskini.Amesema serikali pamoja na wadau wanaotoa fedha kwa kaya maskini,ili ,ziweze kujikwamua kutoka lindi la umaskini.

“Njia mojawapo ya kuzisaidia kaya hizi maskini kuboresha vipato vyao,ni hii ya miradi midogo midogo ya ufugaji kuku,mbuzi na mifugo meinge.Ninyi maafisa mifugo ambao mpo karibu na kaya hizi,zisimamieni kikamilifu,msisubiri mfuatwa,ninyi ndio muifuate miradi huko iliko”,alisisitiza.Aidha, mkuu huyo wa mkoa, amewataka watendaji hao wahakikishe wana simamia watoto wa kaya maskini wana hudhuria shuleni bila kukosa.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (anayeangalia kamera) akimpatia Nya Mathias shilingi 34,500 kama malipo ya kuchimba bwawa kwa siku 15 ambapo kila siku anapaswa kulipwa shilingi 2,300. Fedha hizo zimetolewa na TASAF 111 kwa ajili ya kunusuru kaya maskini kupitia miradi ya jamii iliyoibuliwa na walengwa wa TASAF.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiangalia bwawa linaloendelea kuchimbwa na kaya maskini za kijiji cha Kikonge wilaya ya Iramba kupitia TASAF 111. Mkuu huyo wa mkoa ameagiza halmashauri zote zisaidie kutoa fedha ili ujenzi wa mabwawa yaliyoibuliwa na kaya masikini yaweze kukamilika kwa muda mfupi.
Mkazi wa kijiji cha Kikonge wilaya ya Iramba Mkoani Singida Stephano Mkiya akizungumza muda mfupi kabla ya zoezi la kuhaulisha fedha za TASAF 111 za kunusuru kaya maskini amesema kupitia fedha za TASAF ameweza kuanzisha ufugaji wa mbuzi na pia anamudu kuwasomesha watoto wake.
Mkazi wa kijiji cha Kikonge wilaya ya Iramba Mkoani Singida Elizabeth Mkumbo akizungumza muda mfupi kabla ya zoezi la kuhaulisha fedha za TASAF 111 za kunusuru kaya maskini, Elizabeth amesema kupitia fedha za TASAF ameweza kujenga nyumba bora ya mabati na kwa sasa ana uhakika wa chakula tofauti na kipindi hajaunganishwa na mpango wa TASAF.
Mratibu wa TASAF Mkoani Singida Patrick G. Kasango akizungumza muda mfupi kabla ya zoezi la uhaulishaji wa fedha za TASAF 111 za kunusuru kaya maskini 146 katika kijiji cha Kikonge wilaya ya Iramba mkoani hapa. Kwa mujibu wa Kasango hadi sasa kaya 39,102 maskini Mkoa wa Singida zimenufaika kwa kupatiwa zaidi ya shilingi bilioni 20.3.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...