Wafanyakazi wa Serikalini Wilayani Handeni wametakiwa kutoa ushirikiano kwa namna yoyote ile kama kuna eneo wanatakiwa kutoa ushahidi Mahakamani. Wametakiwa kuhudhuria mahakamani ili waweze kusaidia haki iweze kupatikana kwa wakati.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe alipokuwa akihutubia wananchi na wataalamu mbalimbali kwenye ukumbi wa Mahakama ya Wilaya ya Handeni jana katika maadhimisho ya siku ya sheria Nchini iliyoandaliwa na Mahakama ya Wilaya mwaka 2017 yenye kauli mbiu ya “ umuhimu wa utoaji haki kwa wakati kuwezesha ukuaji wa uchumi”.
Gondwe alisema “amani na utulivu ndio matunda ya Haki, sehemu yeyote iliyokosa amani na utulivu basi lazima kuna haki imepokonywa” Kuli mbiu yetu inatukumbusha wadau wote ambao tunasimamia sheria kuanzia jamii ya kawaida , wataalamu, mawakili, wanasheria ,TAKUKURU, uhamiaji na magereza tuweze kufanya kazi kwa pamoja ili haki iweze kutendeka kwa wakati na kukuza uchumi wetu.
Aidha alieleza kuwa TAKUKURU, Magereza, Uhamiaji , Wanasheria na Mawakili wa Serikali na kujitegemea hawataweza kufanikiwa katika kupambana na Rushwa na kutoa haki kama Mahakama haitakuwa mdau mkuu katika hili. Alisema kuwa kwa kuliona hilo Mahakama imetoa elimu kwa wananchi wiki nzima juu ya umuhimu wa utoaji wa haki kwa wakati kuwezesha ukuaji uchumi.
Mahakama yenyewe imefahamu nafasi ya kusimama na kuweza kushirikiana na wadau wote ili kuhakikisha kwamba wananchi wanoishi Handeni wanapata haki mbali na changamoto mbalimbali zinazoikumba Mahakama hasa ukosekanaji wa watoa ushahidi hali inayopelekea kuchelewa kwa kesi na maranyingine kufungwa kwa kukosa ushahidi uliojitosheleza. Mwananchi anapodai haki lazima afahamu kuwa anao wajibu wa kufanya ili haki hiyo aweze kuipata, alisema Mh. Gondwe.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe akihutubia wananchi na viongozi mbalimbali kwenye maadhimisho hayo
Afisa upelelezi Bw. Paul Kimaro akitoa hotuba fupi wakati wa maadhimisho ya sheria
Mkuu wa Wilaya na wataalamu mbalimbali wakati wa wimbo wa Taifa.
Waendesha mashtaka wa Wilaya ya Handeni Bw.Joseph Hamisi na Nzagalila Kikwelele wakisikiliza hotuba wakati wa maadhimisho.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wikaya ya Handeni Bw. Noel Abel akisalimia wananchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...