Na Mwandishi wetu
Taasisi ya Global Peace Foundation (GPF) Tanzania, imemteua mshindi wa Big Brother Africa Hotshots 2014) Idris Sultan, kuwa balozi wa amani kwa vijana duniani.
Mkurugenzi Mkazi wa GPF Tanzania, Martha Nghambi alisema kuwa wameamua kumtumia Idris kutokana na mvuto wake kwa vijana na kutokana na hilo atafikisha ujumbe kirahisi kwa vijana ambao ni zaidi ya asilimia 60 ya idadi ya watu Tanzania.
Alisema kuwa bado kuna changanoto nyingi za kudumisha amani duniani kwani mpaka sasa kuna baadhi ya nchi zipo katika matatizo makubwa yaliyosababishwa na uvunjifu wa amani.
Martha alisema kuwa Idris ni mtu sahihi katika kampeni yao na wanaamini kuwa kupitia yeye vijana na watu wengine watapata ujumbe wa kuhamaisha kudumisha amani duniani.
 “Kuna baadhi ya nchi zina matatizo ya amani, waswahili wanasema, ukiona kwa mwenzako kunawaka moto… kwako andaa maji, sisi tumeamua kuchukua tahadhari mapema ili kulinda amani yetu,”
Kwa upande wake, Idris alifurahi sana kupewa nafasi hiyo ambayo ni kubwa sana katika maisha yake.
“Wamenithamini na kuniona ninafaa katika kampeni hii, ni kweli, amani inatakiwa kuanzia kwenye familia mpaka juu ambako wengi wanadhani vita tu ndiyo inatakiwa kupigiwa kelele,  vijana ndiyo nguvu kazi ya ya taifa na hivyo tunatakiwa kuwa na mawazo yaliyopanuka ili kujipatia vipato na kuachana na lawama kutokana na kukosa soko la ajira,” alisema Idris.
Alifafanua kuwa kuwa balozi ni jukumu zito na atalitumikia ipasayo ili kufikia malengo yaliyowekwa. “Amani ni  kazi ya kila siku na ni muhimu, leo hii wasanii wanaigiza na wanamuziki wanafanya kazi zao bila kuwa na woga, hii yote inatokana na amani,” alisema.
Global Peace Foundation ni shirika lisilo la kiserikali na lisilo tengeneza faida lenye makao yake makuu, mjini Washington DC, Marekani. Shughuli kubwa la shirika hili ni kuhamasisha amani duniani kupitia matawi yake mbalimbali duniani.
Mbali ya Tanzania, matawi mengine katika bara la Afrika ni Kenya, Uganda na Nigeria. Kauli mbiu ya shirika hilo ni “We are all  “One family under God”(sisi wote ni familia moja kwa Mungu).
Kwa sasa Global Peace Tanzania inaendesha kampeni ya kuhamsisha amani kuanzia ngazi ya familia ijulikanyo kama “Vijana na Amani”. Kupitia kampeni hii, GPF Tanzania inahamasisha amani kwa kutoa elimu katika shule, vyuo na jamii kwa ujumla.

 Mshindi wa Big Brother Africa Hotshots 2014) Idris Sultan (kulia), akipokea cheti cha utambulisho  wa kuwa balozi wa Amani kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi Taasisi ya Global Peace Foundation (GPF) Martha Nghambi.
Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Global Peace Foundation (GPF) Tanzania, Martha Nghambi (wa pili kushoto) na mshindi wa Big Brother Africa Hotshots 2014) Idris Sultan (wa tatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutangazwa kuwa balozi wa amani kwa vijana Tanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...