Na Anthony John, Globu ya Jamii
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam , limesema Jalada la kesi ya kukutwa na bangi Msanii maarufu na Mlimbwende , Wema Sepetu bado linapitiwa na Mwanasheria wa Serikali na baada ya kukamilika kwa upelelezi atapelekwa mahakamani.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi Simon Sirro amesema jeshi la polisi limeshafanya kazi yake hivyo taratibu za kisheria za kesi ya Msanii huyo zinaandaliwa kwa ajili ya kumfikisha mahakamani.
Amesema katika mapambano ya dawa kulevya, wananchi na raia wema wameaswa kuacha kutoa habari za uvunjifu wa amani katika mkoa wa Dar es salaam,badala yake wajikite kutoa taarifa zilizokuwa za kweli.
"Unapotoa taarifa ambazo si za kweli haumdanganyi kamishina Sirro ,unakuwa unalidanganya Jeshi la polisi ,kwa ujumla naomba raia wema waendelee kutoa taarifa lakini watoe taarifa za uhakika"amesema Sirro.
Pia Siro ameongeza kuwa Jeshi la polisi limejipanga vizuri kwa kuwapokea watakao fika siku ya ijumaa lakini kikubwa wafike waje waripoti.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...