Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Diwani wa kata ya Mbagala Kuu Yusuf Manji amesema amepata taarifa ya kuitwa kupitia vyombo vya habari kuwa anaitwa katika kituo cha Kati kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na kushukiwa kuwa na matumizi au uuzaji wa dawa za Kulevya .
Manji ambaye pia ni Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, amesema kuwa kama Mkuu a Mkoa anataka msaada wa kutajiwa majina ya wahusika basi asingemuita kwa kutumia vyombo vya habari kwani anahatarisha maisha yake .

Kutokana na hilo, Manji amesema kuwa yeye hatasubiri Ijumaa kwenda kuhojiwa Zaidi kesho asubuhi ataenda ili kujua anaitiwa nini ,kwani yeye ana kazi zake na hawezi kubadili ratiba, isitoshe wameitwa watu 65 kufika siku ya Ijumaa saa 5 na kutaka kujua watahojiwa kwa muda na kama akiingia mapema watasema ametoa rushwa.

Mbali na hilo ameenda mbali Zaidi na kusema kuwa amechafua jina lake na kwa suala hili na nikishatoka polisi nitamshitaki kwa udhalilishaji huu ili nipate haki yangu kwani kunichafua mimi ni sawa na kuichafua klabu ya Yanga, na kama wanachama wa Yanga hawana imani na mimi waandike barua ya kutokuwa na imani na mimi na nitjivua uongozi. 

“katiba inasema kila mtu ana haki yake, ukinichafua mimi kama Mwenyekiti wa Yanga unachafua Yanga nzima, na kama wanachama wa Yanga hawana Imani na mimi waandike barua ya kutokuwa na imani na mimi,”amesema Manji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. yusuf Amelipa mabillions ya hela kwenye Tax (ushuru) - Ndio anatakiwa alipo polisi #isupportYusufManji

    ReplyDelete
  2. Amefanya la maana sana kuitikia mwito wa mkuu wa mkoa,Anastaili sifa na ni mfano wa kuigwa

    ReplyDelete
  3. 1.Vita zidi ya madawa ya kulevya ni vita ngumu. kwa nini ni mkoa wa DSM peke yakee.
    2.Je Tanzania inaiga Rodrigo Duterte rais wa Philippines anakamata na kupiga risasi hapohapo wauza na watumiaji wa madawa ya kulevya?
    3. Kwani mtu ukilipa tax (ushuru)eg Manji,Waziri, mbunge etc hutakiwi uitwe Polisi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...