Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira,
akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Watanzania wanaorudishwa nchini
kutoka Msumbiji. Rwegasira amesema Uhusiano kati ya Tanzania na Msumbiji unaendelea
kuimarika kila siku, hivyo aliwataka Watanzania wafuate Sheria za Uhamiaji za
nchi hiyo kwani zoezi linalofanyika nchini humo halijawalenga Watanzania pekee
bali raia wote wanaoishi na kufanya kazi bila kufuata taratibu za kisheria
nchini humo. Aidha, amewataka wananchi kutolikuza tukio hilo bila sababu za
msingi. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dar es
Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi.
Home
Unlabelled
KATIBU MKUU RWEGASIRA: UHUSIANO KATI YA TANZANIA NA MSUMBIJI BADO UPO IMARA, AWATAKA WATANZANA KUFUATA SHERIA ZA UHAMIAJI NCHI WANAZOISHI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...