Baada ya serikali kusitisha agizo la Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) lililokataza TV za mitandaoni zisiendelee kutoa huduma, Michuzi TV imerudi hewani kwa kishindo huku ikiwaahidi wadau wote kwamba mambo sasa yatakuwa motomoto kuliko ilivyokuwa awali.
Serikali imesitisha agizo hilo la TCRA baada ya kuonekana halina mantiki kwa vile kanuni za namna ya kuendesha huduma hii hazipo tayari na kuzuia ni kutowatendea haki wananchi wanaofurahia huduma hii bila malipo. Michuzi TV itaendelea kupiga mzigo huku ikisubiri na hatimaye kutii kanuni zozote zitazowekwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...