Katibu Mkuu wa Shirika la Forodha Duniani (World Customs
Organisation-WCO) Dk. Kunio Mikuriya akisisitiza jambo wakati
wa kikao cha pamoja na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata (kulia) alipotembelea TRA ili
kujadili masuala mbalimbali na kuona maendeleo ya miradi ya
Forodha inayotekelezwa na TRA kwa ushirikiano na WCO
Katibu Mkuu wa Shirika la Forodha Duniani (World Customs
Organisation-WCO) Dk. Kunio Mikuriya (kulia) akifurahia zawadi
ya kitabu cha historia ya Tanzania ambacho Kamishna Mkuu wa
TRA Bw. Alphayo Kidata alimkabidhi kama ishara ya ukumbusho
wa ziara yake nchini Tanzania. Dk. Mikuriya alitembelea TRA ili
kujadili masuala mbalimbali na kuona maendeleo ya miradi ya
Forodha inayotekelezwa na TRA kwa ushirikiano na WCO.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Bw. Alphayo Kidata (kulia) akisalimiana na Katibu Mkuu wa
Shirika la Forodha Duniani (World Customs Organisation-WCO)
Dk. Kunio Mikuriya alipotembelea TRA ili kujadili masuala
mbalimbali na kuona maendeleo ya miradi ya Forodha
inayotekelezwa na TRA kwa ushirikiano na WCO
Meneja Mifumo ya Kielektroniki ya Forodha kutoka
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tinkasimile Felix
(aliyesimama) akitoa maelezo ya jinsi Mfumo wa Forodha
(TANCIS) unavyofanya kazi kwa Katibu Mkuu wa Shirika la
Forodha Duniani (World Customs Organisation-WCO) Dk. Kunio
Mikuriya (aliyeketi katikati). Wengine ni Meneja wa Maendeleo
Ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini kutoka Shirika la Forodha
Duniani Bw. Patrick Gyan (kushoto) pamoja na Kamishna wa
Forodha na Ushuru wa Bidhaa Bw. Jocktan Kyamuhanga (kulia).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...