KATIKA kuadhimisha miaka miwili tangu kuanzishwa kwake, Kipindi  bora cha Michezo nchini Tanzania cha Sports headquarters, kinachorushwa na EFM Radio kila siku za Jumatatu hadi ijumaa, saa 3:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana, kikiwa na watangazaji nguli wa michezo wakiongozwa na Maulid Kitenge na mchambuzi mkongwe wa soka Ibrahim Masoud (Maestro)  kitasheherekea kutimiza miaka miwili siku ya Ijumaa tarehe 24/02/017.

Maadhimisho hayo yataenda sanjari na matangazo ya moja kwa moja ya mchezo wa soka kati ya watani wa jadi Yanga FC na Simba SC yatakayo rushwa siku ya Jumamosi tarehe 25/02/2017 kuanzia saa 10: 00 jioni. 

Shamrashamra hizo zitawezeshwa na Benki inayosaidia jamii kukua kiuchumi ya DIAMOND TRUST 

Mwaka huu wa pili wa kipindi hichi umekua wa mafanikio zaidi kwani kimefanya mapinduzi ya kurusha matangazo yake live mtaani, imezindua kikundi cha jogging ikiwahusisha wadau wake na vilevile imewapa fursa wasikilizaji wake pamoja na wapenzi wa michezo kuchambua mechi za kimataifa na kitaifa  moja kwa moja katika bar-Mida ya kubeti ,vile vile imewapa fursa baadhi ya watangazaji wa kipindi hicho kutambulika kimataifa kwa kupitia stesheni ya Super sports.

EFM Radio inaendelea kuwashukuru wasikilizaji wake na daima  itaendelea kuwapa burudani, taarifa na elimu kupitia vipindi vyake mbalimbali .

“EFM RADIO …….NI KWIKWI”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...