Na Bartholomew John Wandi
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawawahakikishia Umma wa Watanzania kuwa hakuna kura yoyote inayoibiwa sikuwa ya kupiga kura, iwe Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani au Uchaguzi Mdogo wa Ubunge au Udiwani.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchagzi, Kailima Ramadhan Kombwey wakati alipokutana na Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Pulisher waliotaka kujua Mchakato wa Uchaguzi hadi kuhesabu kura na kumtangaza Mshindi.
Watu wengi vikiwamo vyama vya Siasa huwaminisha Wafuasi wao kuwa wakati wa kupiga kura huibiwa kura zao ndiyo maana huwashawishi wafuasi wao kulinda kura zao kitu ambacho hakipo
Mkurugenzi alieleza kuwa Kabla ya siku ya Kupiga Kura, Vyama vyote vya Siasa vilivyosimamisha wagombea wao wa Urais,Ubunge na Udiwani huagizwa kuleta Mawakala wao wa Kulinda kura zao na maslahi ya Vyama vyao vya Siasa na kuwa makini na mchakato unavyoendelea Kituoni.
Mara nyingi Mawakala wanatakiwa kutoka katika maeneo wanayoishi ili kubaini mtu ambaye hawamfahamu asiweze kupiga kura kwa kutumia kadi ya mtu mwingine.
“Baada ya Mpiga Kura Kumpa Kadi ya Kupigia Kura, Msimamizi wa Msaidizi wa Kituo baada, hutafuta jila la Mpiga Kura huyo na anapoliona hulisoma kwa sauti kubwa ili Mawakala wa Vyama nao wasikie na kuhakikisha anayeitwa jina hilo ndye mwenyewe au siye?” alisema Mkurugenzi wa Uchaguzi.
Kama anayeitwa jina ndiye Mpiga Kura Mwenyewe huruhusiwa kuendelea na Mchakato wa Upigaji kura lakini kama Mawakala wakiona siye mwenye jina hilo na wana ushahidi wa kutosha humzuia asipige kura.
Mara nyingi pia baadhi ya mashabiki na wafuasi wa Vyama vya Siasa huvumisha kuwa watu waliokufa majina yao wameonekana yametikiwa kuonyesha kuwa jina lake limetumiwa na mtu mwingine kupiga kura kuonyeha kuwa sio kweli kwa sababu Mawakala wa Vyama hivyo vya Siasa wangembaini.
Mkurugenzi alibainisha kuwa siyo jambo jema kwa Wakala wa Chama cha Siasa kukataa kusaini Matokeo ya Uchaguzi ya awali yanapotangazwa kituo cha Kupigia Kura, Kwenye Kata baada ya Kujumlishwa na Kumtanga Mshindi wa Udiwani au Jimboni anapotangazwa Mshindi wa Ubunge au au Makao Makuu ya Tume anapotangazwa Mshindi wa Urais kwa sababu kwa sababu muda wote alishiriki hatua zote na hajaona mahali popote alipoona aliibiwa kura.
Aidha, Murugenzi alisistiza kuwa kutosaini kwa Wakala wa Chama hakumzuii Mwenyekiti wa Uchaguzi kutomtangaza Mshindi wa Kiti cha Urais, Msimamizi wa Uchaguzi Ngazi ya Jimbo kutomtangaza Mshindi wa Kiti cha Ubunge au Msimamizi Msaidizi Ngazi ya Kata kutomtangaza Mshindi wa Udiwani.
“Pamoja na hayo, hakuna hata siku moja Mawakala wa Vyama vya Siasa waliowahi kuleta ushahidi wao wa Matokeo ya awali vituoni Tume na kulalamika kuwa matokeo yaliyotangazwa ni tofauti na niliyo nayo”. Alisema Kombwey.
Mkurugenzi wa Uchaguzi alimalizia kwa kuwapa Wafanyakazi wa Global Publisher nafasi ya kufanya onyesho la Upigaji Kura Kituoni kwa kushiriki wenyewe nafasi zote kuanzia Mawakala, Msimamizi wa Kituo, Msimamizi Msaidizi wa Kituo na Wapiga Kura, Ujumlishaji wa Kura za Awali Kituoni za Ubunge Mpaka Jimboni na Kumtangaza Mshindi wa Kiti cha Ubunge.
Wafanyakazi hao wa Global Publisher walipata kufahamu kuwa Mchakato wote waliofanya Kituoni hakuna mwanya wowote ulioonekana kwa Chama Chochote cha Siasa kuiba Kura au kuibiwa kura au Mtu ambaye siyo wa Kituo hicho kuruhusiwa kupiga Kura.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...