Na Karama Kenyuko, Globu ya Jamii .

Mbunge wa Singida Mashariki ,Tundu Lissu amewasilisha maombi ya dhamana Mahakama kuu baada ya polisi kumnyima dhamana hiyo pamoja na kushindwa kumpeleka mahakamani licha ya kukaa kituoni hapo toka jana.

Maombi hayo yamewasilishwa na wakili wake, Peter Kibatala leo mchana katika Mahakama Kuu.

Amesema wamepeleka maombi Mahakama Kuu iingilie kati ikiwezekana impe dhamana yenyewe kwa sababu wanaamini mahakama kuu inauwezo kwenye mazingira kama hayo ambapo polisi wamekataa kumpa dhamana na masaa 48 yanaisha bila kumleta mahakamanii.

Kibatala amesema hayo leo jioni wakati akiwapa taarifa fupi waandishi wa habari walioshinda mahakamani hapo tokea asubuhi wakimsubiri Tundu Lisu kufikishwa kizimbani.

Mara baada ya muda wa mahakama kuisha jioni ya leo bila mteja wake kuletwa mahakamani, wakili kibatala alisema, mteja wao (Lisu) analalamikia mambo kadhaa ya kisheria likiwemo suala la kukamatwa bila ya waliomkamata kuwa na hati ya kumkamata (arrest warrant).Aliongeza kuwa, Lisu aliwaeleza pia alikamtwa akiwa katika shughuli za bunge, bila ya spika wa bunge kufahamu. 

Alisema Lisu aliwaeleza kuwa hata polisi waliomkamata alikuja kuwatambua kuwa ni polisi wa kweli njiani, pale alipokuwa akikamatwa alimtambua polisi mmoja tu ambaye ni RCO wa Dodoma kwani hata utambulisho wao haukuwa na imani nao.

Aliongeza kuwa mara baada ya kumkamata walimsafirisha usiku kwa usiku kana kwamba ni mhalifu mkubwa, wakati ni mtu anayefahamika, “ni wakili, mkongwe, mbunge na mnadhimu mkuu kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni lakini bado polisi wamemnyima dhamana”.

Aliongeza kuwa walitegeme leo angeletwa mahakamani lakini mpaka sasa hajaletwa, kwa hiyo tumepeleka maombi mahakama kuu iingilie kati ikiwezekana impe dhamana yenyewe kwa sababu tunaamini mahakama kuu inauwezo kwenye mazingira kama haya ambapopolisi wamekataa kumpa dhamana na masaa 48 yanaisha bila kumleta mahakamai.

Kama wao walikuwa na mwezi mzima wa kupepeleleza kwa nini hawaleti mahakama. Tunatemea mahakama kuu kesho watasikiliza maombi ya dhamana au wale wanaohusika waandae majalada wamlete mahakamani tuendeshe kesi.
 Wakili wa mbunge,Tundu Lissu,Peter Kibatala akizungumza na waandishi wa habari katika viunga vya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo jijin Dar es Salaam. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...