Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya uchukuzi), Eng. Dkt.
Leonard Chamuriho ameipongeza kampuni ya huduma za meli nchini (MSCL), kwa
kukarabati meli zake kwa kutumia fedha za ndani na hivyo kuhuisha utendaji kazi wa
kampuni hiyo.
Akizungumza jijini Mwanza mara baada ya kukagua huduma zinazotolewa na kampuni
hiyo Eng. Dkt. Chamuriho amesema Serikali itawekeza kikamilifu kwenye kampuni hiyo
baada ya kuridhika na utendaji uliopo sasa.
“Fanyeni kazi kwa bidii na fikra mpya Serikali inashughulikia kwa karibu suala la
mishahara yenu na stahili nyingine” amesema Eng. Dkt. Chamuriho.
Hivi karibuni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa
alimteua Kaimu Meneja Mkuu mpya wa kampuni hiyo Bw. Eric Hamisi ambaye kwa
kushirikiana vema na menejimenti na wafanyakazi wamewezesha kuongeza mapato
kwa kwa asilimia 100.
Kampuni ya huduma za Meli MSCL ni moja ya kampuni ya Meli yanayomilikiwa na
Serikali kwa asilimia 100 na kusimamiwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Sekta ya Uchukuzi na inatoa huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo
katika maziwa makuu yaliyopo nchini Victoria,Nyasa na Tanganyika
Meli ya MV. Clarias inayomilikiwa na Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), inayofanyiwa
ukarabati katika bandari ya Mwanza ambao ukarabati wake utakamilika mwanzoni mwa wiki
ijayo na kuanza kutoa huduma mwishoni mwa mwezi huu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Sekta ya Uchukuzi, Eng.Dkt,
Leonard Chamuriho, akitoa maelekezo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za
Meli (MSCL), Bw. Eric Hamisi (mwenye shati jeupe), wakati alipokagua ukarabati wa Meli
ya MV. Clarias.
Fundi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), akiendelea na ukarabati wa meli ya MV
Clarias ambayo ukarabati wake utakamilika mwishoni mwa wiki na kuanza kazi ya
kutoa huduma katika Ziwa Victoria.
Nahodha wa Meli ya Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Swedi Ruganza akitoa
maelezo ya namna nahodha anavyoendesha meli kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano. Sekta ya Uchukuzi, Eng. Dkt. Leonard Chamuriho (katikati),
alipofanya ukaguzi wa ukarabati wa meli hiyo jijini Mwanza.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Sekta ya Uchukuzi, Eng.Dkt.
Leonard Chamuriho, akitoa maelekezo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Huduma za Meli (MSCL),
Bw. Eric Hamisi (wa pili kutoka kushoto), mara baada ya kuangalia kina cha maji katika
bandari ya Mwanza.
PICHA NA Biseko Lisso Ibrahim, WUUM (U)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...