Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo Zamaradi Kawawa akizungumza juu ya Bonanza hilo
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Theophil Makunga akizungumza na waandishi wa habari juu ya Tamasha hilo
Na Humphrey
Shao, Globu ya Jamii
Waziri wa
habari Sanaa, utamaduni na Michezo, Nape Nnauye anataraji kuongoza Bonanza la mazoezi na upimaji afya February
18 mwaka huu ulionadaliwa na Chama cha maofisa mawasiliano Serikalini (TAGCO)
kwa kushirikiana na jukwaa la wahariri Tanzania na Dar es Salaam City Press
Club.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Msemaji wa chama TAGCO, Abel
Ngapemba ametaja kuwa lengo la Bonanza hilo ni kuhamasisha wananchi kujenga
tabia ya kufanya mazoezi na kupima afya kama ilivyozoeleka kwa kuunga mkono
kampeni iliyozinduliwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.
“washiriki
wa bonanza hili ni pamoja na maofisa mawasiliano wa Serikali na wasekta binafsi
,Wahariri , Wahandishi wa habari na Bloggers na wananchi kwa ujumla kwa
kuongozwa na Waziri Nape Nnauye na kuhudhuliwa na viongozi wa Wizara ya afya na
ustawi wa jamii, jinsia wazee na watoto” amesema Abel.
Ametaja kuwa
mbali ya mazoezi taasisi zitakazo shiriki kutoa huduma siku hiyo ni pamoja na
Tasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Hospitali ya Saratani ya Ocean Road,Hospitali
ya Sanitas,CCP Medicine Kinyerezi na Mfuko w Bima ya Afya (NHIF), Chama cha
madaktari wa meno Tanzaniana tasisi ya wagonjwa wa mifupa MOI.
Abel ametoa
wito kwa wahariri wa vyombo vya habar, waandishi wa habari , Bloggersna maofisa
mawasiliano Serikalini, mashirika binafsi na tasisi za kimataifa kujitokeza kwa
wingi katika bonanza hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...