Shirikisho
la Mpira wa Miguu (TFF), limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za vifo vya
mashabiki 17 na wengine kujeruhiwa katika tukio la watu kukimbia uwanjani kwa
tishio la mabomu wakati wakati wa mchezo wa timu mbili zenye ushindani.
Maelfu ya
mashabiki, wakiwamo watoto wadogo walianza kukimbia na wengine kukanyagana hali
iliyosababisha vifo uwanjani.
Rais
Jamal Malinzi wa TFF, ameelezea kushtuka kwa taarifa hizo za vifo hivyo
vinavyoripotiwa kutokea Ijumaa Februari 10, 2017 kwenye Uwanja wa Angola ulioko
mjini Uige, Kaskazini mwa nchi hiyo.
Kwa masikitiko
makubwa, Rais wa TFF Malinzi ametuma salamu zangu za rambirambi kwa Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Angola (AFF); familia za ndugu waliopoteza
wapendwa wao katika maisha, watu wa nchi hiyo, kutokana na vifo hivyo.
Rais
Malinzi amesema kwa nguvu za Mungu anawaombea heri ya kupona majeruhi na kwamba
Tanzania inasali kuwaombea watu wa Angola wakati huu mguu.
Mwenyezi
Mungu azipokee roho za marehemu mahali pema peponi.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA
MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...