Na Stella Kalinga
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu,Ndg.Jumanne Sagini ametoa
wito kwa viongozi na Wakuu wa Taasisi za Umma mkoani humo, kusimamia utekelezaji wa agizo la Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan la kufanya
mazoezi ya viungo Jumamosi ya pili ya kila mwezi.
Sagini ametoa wito huo leo katika hotuba yake kwa
watumishi wa umma,wanafunzi na wananchi walioshiriki mazoezi ya viungo na
michezo mbalimbali katika uwanja wa Halmashauri ya Mji Bariadi ikiwa ni
utekelezaji wa agizo la Mhe.Makamu wa Rais.
Amesema Simiyu wamejipanga kutekeleza na akawataka
watumishi wa Umma kuheshimu agizo hilo na kutekeleza kama ilivyoelekezwa, badala
ya kuamua kushiriki au kutoshiriki.
"...Niombe wote wanaowasimamia Watumishi wa Umma
kuhimiza utaratibu huu wa mazoezi ambao ni agizo la Makamu wa Rais ambalo limeongozana
na nyaraka za Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara yenye dhamana na Elimu na Mafunzo
ya Ufundi, lakini mara kadhaa hata Wizara ya Afya imekuwa ikisema, Sisi
kama Watumishi wa Umma hatuwezi kuchagua kutekeleza au tusitekeleze"
alisema.
Amesema kila mkuu wa Taasisi,Idara,Sehemu anapaswa
kuhakikisha watumishi walio chini yake wanashiriki mazoezi ya viungo mwezi
ujao(Machi) kwa kuwa kushindwa kutekeleza Maelekezo ya viongozi pasipo
sababu za msingi ni utovu wa nidhamu, ambalo ni kosa kwa mujibu wa
Sheria,kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma.
Katibu
Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini (mwenye kofia nyeupe) akiwa na baadhi
ya watumishi katika mazoezi ya kutembea
kwenye Uwanja wa Halamshauri ya Mji Bariadi, wakati wa utekelezaji wa agizo la
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan la
kufanya mazoezi ya Viungo.
Katibu
Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini (wa pili kushoto) akishiriki mazoezi
ya viungo na baadhi ya watumishi wa
Umma,wanafunzi na wananchi katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji Bariadi.
Timu
ya Sekretarieti ya Mkoa ikivuta kamba dhidi ya timu ya Halmashauri ya Mji
Bariadi (haipo pichani) katika Uwanja wa
Halmashauri ya Mji Bariadi.
Katibu
Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini akizungumza na Viongozi na watumishi
wa Umma, wanafunzi na wananchi walioshiriki mazoezi ya viuongo na michezo
mbalimbali mjeni Bariadi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan.
Baadhi
ya watumishi wakishiriki mbio za mita 100 wakati wa utekelezaji wa agizo la
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan la
kufanya mazoezi ya Viungo na michezo mbalimbali mjini Bariadi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...