
Ijumaa kutakua na mada inayohusu fursa za mitandaoni, changamoto na vitisho vinavuyoigusa tasnia ya muziki. Kutoka kwenye jopo la wageni Jude Clark, mwanzilishi wa Joose Digital na Eddie Hatitye, Mkurugenzi wa Music in Africa wataongelea ujuzi wao kwenye maeneo ya hatimiliki, utandawazi, digitali, soko la muziki duniani na maswala ya teknolojia ya mitandao.
Kwa kutambua uwezo wa kidigitali ni muhimu kwenye taaluma, wahudhuriaji watashuhudia nguvu ya mitandao ya kijamii ilivyo na nguvu ya kuunganisha mashabiki na wawekezaji, na kuongeza masoko kwa kutumia mitandao ya kijamii.
Wanamuziki hujikuta mstari wa mbele kwenye harakati maarufu kwa kutumia sauti zao kwa niaba ya wasiosikika. Wakati mwingine wasanii hujikuta hatarini baada ya ujumbe wa muziki wao kuwatuhumu wasikilizaji na wenye mamlaka. Msanii anawezaje kutumia uhuru wa kuongea na kufungiwa kitaaluma?
Mada ya Jumamosi itaeleza mtazamo huru wa ubunifu Afrika, ripoti imeandikwa na waandishi 25 kutoka Nchi 14 na kuchapishwa kwa ushirikiano wa Artwatch Afrika kama sehemu ya mtandao wa Arterial, wenye lengo la kulinda uhuru wa kujieleza. Jopo litajumuisha Nelson Mandela wa kundi la Sarabi Kenya, Mamou Daffe – Mkurugenzi,Tamasha la sur le Niger, Mali na Dr. Omar Abdalla Adam –Mkurugenzi, Bodi ya Udhibiti Zanzibar.
Jumapili wasanii wa tamasha wanakaribishwa kwa maswali na majibu ya kina. Washiriki wanatarajiwa kuwa Pat Thomas and Kyekyeku kutoka Ghana, Roland Tchakounte kutoka Cameroun, Bi Mariam Hamdani kutoka Zanzibar and Sahra Halgan kutoka Somaliland. Hii ni sehemu ya kipekee kwa wasanii kutoka bara la Afrika na sehemu mbalimbali kukutana na kubadilishana mawazo. Mada hii itaongozwa na Journey Ramadhan, meneja wa Tamasha.
Movers & Shakers imeandaliwa kutengeneza nafasi za kipekee kwa wasanii na kuwajengea uwezo ili tasnia ya muziki Afrika Mashariki isonge mbele. Mada zitatolewa kila siku kuanzia saa 8:00 mchana mpaka saa 9:30 jioni . Hotel ya Monsoon. Kuingia ni kwa mwaliko tu. Hovyo wasanii na mameneja wa ndani wanahamasishwa kuwasiliana na waandaaji wa tamasha la Sauti za Sauti za Busara kama watapenda kushiriki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...